Bunda
Hali ya afya ya mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la nne, shule ya msingi Bwanza, kata ya Kisorya, wilaya ya Bunda mkoani Mara, aliyeingiliwa na samaki sehemu zake za siri na kukimbilia tumboni inazidi kuimarika.
Mtoto huyo ameibuka nakulielezea tukio hilo kuwa la kihistoria akidai hatalisahau kamwe maishani mwake, daima atalikumbuka na kulisimlia kwa kizazi kijacho wakiwemo wa jukuu kama atajaliwa kuishi maisha marefu kwakuwa nitukio la aina yake, la ajabu, lililomtesa na kumsababishia maumivu makali.
"Nilikuwa nateka maji ziwani, samaki huyo aina ya sato akarukia miguuni mwangu, akaingia sehemu za siri na kukimbilia tumboni, nilijaribu kumvuta lakini sikufanikiwa kwani, alizama kabisa tumboni kupitia sehemu zangu za siri" alisema mtoto huyo ambaye jina lake tunalihifadhi.
Mtoto huyo anayetibiwa kwa mganga wa jadi mwanamke, aliyejitambulisha kwa jina moja la Mshaki baada ya Madaktari wa hospitali za kawaida ikiwemo hospitali ya wilaya ya Ukerewe, mkoani Mwanza kushindwa kutambua tatizo na kumsaidia alisema, samaki huyo alipomuingia sehemu zake za siri, alisikia maumivu makali na kushangaa namna samaki huyo alivyokua akiteleza kuingia ndani tumboni kupitia sehemu zake za siri, kila alipokua akijaribu kumvuta ili amtoe, alihisi maumivu makali zaidi hivyo akalazimika kumuacha na kuzama kabisa tumboni!
"Samaki alipoingia huku chini miguuni na kukimbilia tumboni, niliishiwa nguvu, nilimuita dada Monika niliyekuwa naye ziwani akanisaidia kunishika hadi nyumbani, usiku sikulala, tumbo lilikua likiniuma vibaya mno, kila nilipojisaidia haja ndogo nilikua nikijichungulia na kuona mkia wa samaki huyo ukitokea, hata bibi Emakulata naye alimwona aliponichungulia" alisema mtoto huyo.
Alisema kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kutibiwa na mganga huyo wa kienyeji mkazi wa kijiji cha Amuyebe, Ukerewe mkoani Mwanza japo alisema baada ya kupewa dawa, alitokwa na harufu mbaya sehemu zake za siri mithili ya mzogo wa panya uliooza.
Aidha mganga huyo wa jadi, akizungumza na majira kwa njia ya simu. alikili kumtibu mtoto huyo akidai alichezewa kichawi kwa kuingiziwa dawa tumboni kupitia sehemu zake za siri kwa mwonekano wa samaki, dawa ambayo alisema, ilikua iozeshe viungo vyote tumboni na kumsababishia kifo.
"Mtoto huyu alirushiwa kombora katika mwonekano wa samaki aliyeingia tumboni mwake kupitia sehemu zake za siri, lengo ilikua ni kumuua baada ya kuozesha viungo vyote tumboni lakini, nimemuwahi kabla hajaharibu tumbo lake kwa kumpa dawa ya kumfanya aharishe na kukojoa mara kwa mara, ndiyo sababu anatokwa na harafu mbaya sehemu za siri, ni harufu ya kombora la samaki aliyemuingia, ameoza, na sasa anatoka kwa njia hiyo" alisema mganga.
Bibi wa mtoto huyo Emakulata Mtani (64), aliyedai alikuwa akimchungulia mjukuu wake sehemu zake za siri kila alipokuwa akijisaidia haja ndogo na kumwona samaki huyo akijitokeza sehemu ya mkia alisema, ana furaha kubwa kwa maendeleo mazuri ya afya ya mjukuu wake akiamini kwa hali ilivyo sasa atapona.
Januari mosi, mwaka huu 2014 mtoto huyo akiwa anateka maji katika ziwa Victoria kumwagilia bustani ya nyanya na vitunguu, alidai kurukiwa na samaki aina ya sato sehemu zake za siri, aliyepenya hadi tumboni mwake.
Mtoto huyo alidai kujisikia maumivu makali tumboni na sehemu zake za siri ambapo baba yake mdogo Lenatus Mtani alimpeleka zahanati ya Kisorya, kisha hospitali ya wilaya ya Ukerewe ambapo madaktari walishindwa kumsaidia, aliamua kumpeleka kwa 'mtaalamu' huyo, mkazi wa kijiji cha Amuyebe, Ukerewe mkoani Mwanza, anayemtibu, hali yake ikielezwa kuendelea vizuri.
Miongoni mwa viongozi waliozungumza na majira na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo la aina yake ni mwenyekiti wa kitongoji cha Alwego Leticia Bituro, Diwani wa kata ya Napindi Elias Magoti, kamanda wa jeshi la polisi wilaya ya Bunda (OCD) Mika Nyange.
No comments:
Post a Comment