Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Avery alifanyiwa upasuaji kutokana na matatizo ambayo hayakuwekwa wazi. Mkewe Barbara Avery, alikuwepo hospitali wakati mumewe anakata roho.
Avery alianza kucheza filamu kwenye tamthiliya ya Fresh Price akiwa na Will Smith kuanzia mwaka 1990 mpaka 1996. Muda mfupi tu baada ya mauti yake, msanii mwenzie Alfonso Ribeiro, alitoa taarifa kuhusu kifo chake kwenye mtandao wa twitter.
"Nasikitika sana kusema kwamba James Avery amefariki. Alikuwa ni baba yangu wa pili. Nitamkumbuka sana,” aliandika kijana huyo wa miaka 42 huku akiweka picha ya Avery na Mkewe.
Avery aliendelea kuonekana katika tamthiliya nyingine kwenye televisheni, ikiwa ni pamoja na ya msanii Jamie Foxx, The Division, That ‘70s Show, The Closer pamoja na Grey’s Anatomy.
SEHEMU YA VIDEO YA UNCLE PHIL AKIWA KWENYE TAMTHILIYA YA FRESH PRINCE OF BEL-AIR
No comments:
Post a Comment