Sunday, January 12, 2014

SURPRISE: MTOTO WA NDAUKA APEWA ZAWADI YA AJABU…SOMA HAPA

Msanii wa filamu Tanzania Rose Ndauka aambaye alipata mtoto hivi karibu akiwa salama kabisa yeye na mwanae wamepata zawadi ambayo hawakutegemea kutoka kwa baba wa mtoto hivi karibu.

Maliki Bandawe(pichani akiwa na Rose Ndauka) ambaye pia ni msanii wa musiki wa kizazi kipya alimzawadia mtoto wake nyimbo maalum aliyoitunga na kuingia studio kwaajili hiyo tu.

Kama Jay Z na Beyonce, Malik aliamua kutunga nyimbo maalumu kwaajili ya mwanae wa kike ambaye mpaka tunakwenda mitamboni nyimbo hiyo imeshaanza kuingia sokoni.

SOMA ZAIDI...

Habari kutoka kwa watu walioko karibu na Rose zinasema, Rose alijifungua salama mtoto wa kike tarehe 27 mwezi disemba katika hospitali ya Muhimbili kwa njia ya upasuaji.

Mtoto huyo ambaye amepea jina la Naveen anaendelea kukua na afya njema. Mashabiki na wapenzi wa msanii huyo wa filamu wanamsubiri kwa hamu kubwa Rose ambaye imekuwa ni vigumu sana kuonekana.

Jitihada za kumpata Rose ili kuzungumzia hali yake ziligonga mwamba na hatimae kumpata superstaa aliyekwenda kumjulia hali na kumtakia afya njema katika mafanikio yake na kupokea mtoto wa kike.


Inadaiwa Malik alipatwa na furaha ya ajabu alipo pata taarifa ya kufunga mwaka salama kwa kupata taarifa hizo njema.


No comments:

Post a Comment