Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi Mwandamizi Geoffrey Kamwela ameeleza kuwa ajali hiyo lilitokea jana saa 2:00 asubuhi wakati Gari hiyo aina ya Noah TBUX iliyotoka Itigi kuelekea Mjini Singida, ilipogongana na Lory hilo aina ya Scania T687 AXB. Umbali wa km 60 kutoka mjini hapa.
Alibaini kuwa baada ya ajali hiyo watu 13 wakiwemo wanawake wawili wanaume 10 na mtoto mchanga walikufa hapohapo na miili ya marehemu hao kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mkoa huo.
CHINI: Gari aina ya NOAH T.730 BUX likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana na lori linaloonekana mbele yake upande wa kulia wakati gari hilo dogo likitoka Itigi kwenda Singida na lori likitoka Mwanza kwenda Dar es salaam katika Kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilayani humo.
PICHA ZAIDI…
PICHA ZAIDI…



No comments:
Post a Comment