Mwanamke anayetumiwa kwa kufanya biashara ya watoto katika kijiji cha Ngiresi Wilaya ya Arumeru, Arusha, Martha Ringo, amedaiwa kutoroka chini ya ulinzi wa Kamanda wa kikosi cha Polisi jamii wa kijiji hicho Albert Loyi akisaidiwa na ndugu zake kwa lengo la kumwokoa kuingia katika mikono ya sheria.
Akizungumzia tukio la kutoroka mwanamke huyo, kamanda Albert Loyi amesema baada ya kupata taarifa za siri kuhusiana na Bi. Martha Ringo kutorosha watoto kwa lengo la kuwapeleke mkoani Kilimanjaro kibiashara, alianza kuweka mtego .
Aidha alisema mwanamke huyo anayedaiwa kuwa ana danguro la biashara ya watoto mkoani Kilimanjaro anadaiwa kujihusisha na biashara hiyo pamoja na shughuli zake za uuzaji wa pombe ambapo kupitia watoto hao huweza kuwa dalalia kwa wateja wake.
Kamanda huyo wa polisi jamii aliendelea kusema kuwa kutokana na hatua ya mtuhumiwa kutoroka, kikosi chake kinaendela na operesheni ya kumsaka ili kumkamata na kumfikisha katika vyombo vya dola ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Aliongeza kuwa katika mfululizo wa matukio ya mtuhumiwa kwa nyakati tofauti alibambwa eneo la Sekei katika jiji la Arusha akiwatorosha watoto watano kwa lengo la kuwapeleka mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kibiashara, ambapo watoto hao waliokolewa na wasamaria.
Hata hivyo Mwenyekiti wa kitongoji cha Ngoikaa katika kijiji hicho cha Ngiresi Wilaya ya Arumeru, Elias Lekiringai alipohojiwa kuhusiana na sakata hilo alikanusha tuhuma zilizoelekezwa kwa mtuhumiwa nakudai kuwa baadhi ya wazazi wamekubaliana na mtuhumiwa awatafutie kazi watoto hao.
Kauli hiyo ya Mwenyekiti imepingana na kauli ya kamanda wa polisi jamii Albert Loy aliyesisitiza kauli yake iliyothibitishwa na mwanafunzi aliyenusurika kutoroshwa baada ya mtuhumiwa kumshawishi mwanafunzi huyo aombe pesa kwa wazazi ili akanyolewe nywele hatimaye mtuhumiwa aje kumchukua akiwa saluni hatua ambayo haikuweza kukamilisha lengo na azima ya mtuhumiwa.
Hata hivyo kamanda huyo wa polisi jamii alisema inaonekana yapo mazingira kwa baadi ya viongozi na ndugu zake ya kumlinda mtuhumiwa kutokana na maslahi binafsi ambapo amesisitiza kikosi chake kitaendelea kufanya kazi usiku na mchana ili kukomesha vitendo viovu vinavyofanywa na wahalifu katika kijiji hicho.

No comments:
Post a Comment