Kama haitoshi, sikia hii hapa sasa: hakuna mtoto kuanza shule kabla ya kufikisha miaka 7 (bongo wanaanza wakiwa na miaka 3 mpaka 4, kwa madai wana akili sana), watoto hawapangwi kwa uwezo, eti labda wenye akili kuliko wengine darasa tofauti, kwanza ni kinyume cha sharia( kwetu kuna shule maalumu za wenye akili kuliko wengine – hivi wale wanaishiaga wapi?).
Watoto wanawaita walimu wao kwa majina la kwanza (Tanzania thubutu ndo utakiona cha mtema kuni), na wanafunzi hawapewi homework watakazofanya zaidi ya nusu saa wakiwa nyumbani (hapa nafikiri tunawazidi, maana hakuna kabisa homework labda shule za private).
Cha ajabu sasa: tokea mwaka 2000, Finlad ni kati ya nchi duniani zinazoshika nafasi ya kwanza katika kiwango cha elimu duniani (Tanzania sijui ni ya ngapi).
No comments:
Post a Comment