![]() |
| file photo |
Habari kutoka katika kata hiyo na kuthibitishwa na viongozi wa Serikali, wakiwemo watendaji zinaeleza kuwa mvua hizo zimenyesha mwishoni mwa wiki na kuchukuwa muda wa masaa tisa na kusababisha hasara hiyo,ambayo thamani yake bado haijaweza kufahamika mara moja.
Wakizungumza na mwandishi wa habari, baadhi ya wakazi wa kata hiyo, wakiwemo wale walioathiriwa wameeleza kwamba mvua hiyo, ilianza kunyesha kipindi cha kuanzia saa 8:0 mchana hadi saa 4:0 usiku.
Omari Mbegwa na Zainabu Issa wa kijiji cha Majengo ‘A’na Habiba Hamisi na Bakari Juma wa Makonde wamesema mvua hiyo,ikiambatana na upepo iliweza kusababisha hasara ya majumba na vyakula.
“Unajuwa aridhi ya eneo letu hili limekuwa na tabia ya chemu chemu,mvua ikiwa nyingi basi baadhi ya maji utoka chini na kuja juu na ndivyo ilivyokuwa jana”Alisema Mbegwa.
Zainabu Issa yeye alisema wakati mvua hizo kubwa ziliendelea kunyesha watu waliweza kujihifadhi kwenye majumba yao kwa matarajio ya kusubiri kunyamaza ili waweze kuendelea na majukumu yao,badala yake ilichukuwa muda mrefu bila ya kusimama.
Pia,alisema wakati mvua hiyo ikiendelea kunyesha baadhi ya maji yalikuwa yakitokea aridhi na kuungana na mvua iliyokuwa ikitoka juu na kusababisha ubomoaji wa nyumba zao.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Majengo ‘A’ Safu Hamisi yeye alisema katika vijiji vya Majengo ‘A’na ‘B’ kaya 28 zikiwemo 16 za Majengo ‘A’zimekumbwa na mafuriko hayo.
“Ni kweli ndugu mwandishi tatizo hilo lipo kwenye kijiji changu cha majengo na pia jirani zetu wa ‘B’ nao wamekumbwa na hali hiyo,kwani wao kaya 12 hazina mahali pa kuishi”Alisema Hamisi.
Naye, Afisa mtendaji wa kata ya Mtama,Ally Mohamedi alipoulizwa na gazeti hili,amethibitisha kata yake kukumbwa na mafuriko hayo na kuweza kuleta hasara ambayo iliyopatikana haijaweza kufahamika mara moja.
Mohamedi alivitaja vijiji ambavyo vimekumbwa na mafuriko hayo ni,Makonde,majengo ‘A’na ‘B’ na Mtama yenyewe, na tayari ameshapeleka taarifa ya awali kwa viongozi wa Serikali ngazi ya wilaya,akiwemo mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Lindi vijijini, Selemani Ngaweje na kaimu katibu tawala wa wilaya hiyo, Sharifa Mkwanga nao wamekiri kuwepo kwa tukio hilo na kuahidi kufuatilia ili kuweza kujionea hasara iliyopatikana na hatua za kuzichukuwa.

No comments:
Post a Comment