Tuesday, January 14, 2014

HII INAKUHUSU HUKWEPI : UNAJUA KUWA SIMU YAKO INA KINYESI..!

NDIO, HIYO SIMU YAKO INA KINYESI..!

Habari mbaya kwanza: kuna uwezekano mkubwa kabisa katika simu moja kati ya sita ina kinyesi ndani yake.

Sasa habari njema: wabunifu wawili wanadai wametengeza chaja ya simu ambayo itakundolea huo uchafu.

Katika maonesho ya kimataifa yajulikanayo kama International CES 2014 huko Las Vegas, nchini Marekani, Dan Barnes na Wesley LaPorte wametangaza kubuni chaja ya simu iitwa sabuni ya simu “PhoneSoap”.

PhoneSoap inatumia mionzi ya sumaku(Electromagnetic UV-C) kama ile inayotumika hospitali kuua asilimia 99.9 ya bakteria kwenye simu yako, imeripotiwa na United Press International.

Kwa mujibu wa mtandao wa Time Magazine, vijana hao walivutiwa kuchukua hatua baada ya kuona utafiti wa mwaka 2011 ulioonesha kuwa asilimia 16 ya simu zimejaa uchafu wa kinyesi cha E.coli

Mwanga wa Electromagnetic UV-C unaua bakteria na virusi kwa muda usiozidi dakika 3 mpaka 5, inaweza pia kutumika katika vifaa vidogo vidogo kama simu za kisasa (smartphones) na simu zisizo zidi inchi 6 kwa 4





No comments:

Post a Comment