Picha hiyo inayoonesha ni mpya ambapo mara ya mwisho kutuma picha kwenye ukurasa huo ilikuwa ni mwezi mmoja kabla hajakamatwa.
Picha hizo zimezua mjadala kwa baadhi ya watu huku wakiwa na shauku ya kutaka kujua kama msichana huyo yuko huru, na ni kweli yeye ndiye aliyeituma picha hiyo.
Mwanamitindo huyo ambaye alikamatwa nchini China Desemba 17, akisafirisha dawa aina ya Heroin zenye uzito wa kilo 1.1 kutoka Thailand kuelekea Macao .
Inasemekana kuwa dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na wana usalama kisha kufanyiwa X-Ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vikiwa na thamani ya dola za kimarekani 137,720.
ANGALIA PICHA ZAIDI...
No comments:
Post a Comment