Tunduru
Kijana wa umri wa Miaka 29
mwenye ulemavu wa kushindwa kuongea (Bubu) aliyefahamika kwa jina la Zuberi
Hatima Said anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua Baba yake Mzazi akiwa anamtuhumu kumloga.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki amemtaja Marehemu huyo kuwa ni Hatima Said
Lung’ande (70) na kwamba katika tukio hilo mtuhumiwa alimuua kwa kumpiga na
mpini wa Shoka.
Kamanda Nsimeki aliendelea
kufafanua kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 29 /2013 majira ya Saa 12 Jioni katika kitongoji cha Mchangani
kilichopo katika Kijiji cha Kazamoyo Tarafa ya Lukumbule Wilayani Tunduru
Mkoani Ruvuma.
Alisema kuwa kufuatia hali
hiyo mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani ili sharia iweze kufuata mkondo wake
baada ya kukamilika kwa taratibu za mahojiano yatakayo washirikisha wataalamu
wa Lugha za alama.
Akizungumzia tukio hilo
mkalimani wa familia hiyo Mtoto wa kwanza kati ya watoto wane wa marehemu
Lung’ande Bw.Adamu Sadiki alisema kuwa kabla ya tukio hilo ndugu yake huyo
ambaye ni kati ya watoto watatu wa marehemu wenye ulemavu huo alidaikuwa kwa
muda mrefu amekuwa akimuona marehemu usiku akiwa anamuwangia.
“Tumezaliwa watoto Wanne
katika familia yetu kwa Baba na mama Lung’ande lakini kutokana na mipango ya
mungu wenzangu wote ni mabubu hivyo mimi nimekuwa kiunganishi kikubwa katika
familia, wageni pamoja na ndugu na jama” alisema Bw. Adamu na kuongeza kuwa
Zuberi amekuwa akimlalamika baba kuwa ni mchawi siku za hivi kalibuni hali
ambayo iliwaweka katika mazingira ya utata miongoni mwao.
Mganga aliye ufanyia uchunguzi
mwili wa Marehemu Lung’ande, Dkt. Joseph Ng’ombo alisema kuwa kifo hicho
kilisababishwa na tukio la kutokwa na damu nyingi kufuatia kipigo hicho.
Alisema katika tukio hilo marehemu aliumia vibaya Kichwani upande wa jicho la
kulia pamoja na kupasuka kwa fuvu la kichwa chake na jicho la Kulia kufutia
kipigo hicho.
No comments:
Post a Comment