Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba Wahariri, Absolom Kibanda (New Habari) na Theophil Makunga (Mwananchi Communication - ALIEINUA MKONO) na mwandishi Samson Mwigamba wameachiwa huru na Mahakama ya Kisutu katika mashtaka walioshtakiwa ya uchochezi.
Hatimaye aliyekuwa mhariri wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda na Mhariri Mtendaji wa Mwananchi, Theophil Makunga wameachiwa huru na Mahakama ya Kisutu muda huu. Wahariri hao pamoja na mwandishi wa makala Samsoni Mwigamba walifunguliwa mashitaka ya uchochezi tangu mwaka 2011, kutokana na makala iliyoandikwa na Mwigamba ikisema 'waraka kwa askari wote wa Tanzania' na kuchapwa katika gazeti la Tanzania Daima.
No comments:
Post a Comment