INJINI ya kwanza (PICHANI) kati ya injini 8 ambazo zinatengenezwa na Kampuni ya S.M.H.RAIL ya nchini Malasya leo imefanya safari ya majaribio kuanzia Stesheni ya Mjini Morogoro kwenda Mkoani Dodoma kwa mara ya Kwanza.
Injini hiyo iliyopewa namba 88U01 imeboreshwa kutoka kwenye ile ya awali iliyokua inafahamika kwa namba 8801 na kwa mujibu wa Meneja mradi wa Kampuni hiyo Bw V .Chalapathy injini hii ni ya kisasa zaidi na inatumia teknolojia ya kisasa ikiwa na nguvu ya HP 2300.
Meneja huyo akiwa na timu ya mafundi ambao wameondoka na treni hiyo amesema kwa majaribio injini hiyo itavuta tani 1125 za mzigo ingawa uwezo halisi ni kuvuta tani 1300 kwa mwendo kasi wa Km 50 kwa saa kulingana na uwezo wa reli za hapa nchini na kwamba kwa Malasya injini hii inaweza kwenda umbali wa Km 130 kwa saa kwa kua miundo mbinu ya njia za reli ni mizuri.
“Baada ya injini hii ya leo sasa tunategemea kuendelea kutoa injini moja kila Mwezi,kwa hiyo February tutatoa injini nyingine mpaka mwezi August tutakua tumemaliza Injini zote Nane” alisema Bw Chalapathy.
Amesema jaribio la kwanza lilikua ni kutembeza injini yenyewe bila mzigo kwenda na kurudi Wilayani Kilosa na hili sasa ni jaribio la pili na baada ya hapo wataikabidhi injini hiyo kwa TRL kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na mizigo.
Akizungumzia ubora wa injini hiyo Mshauri wa Mradi huo Bw Wencelaus Kaijage alisema injini hiyo ina mfumo wa udhibiti (Control unit) ambao kwanza unasaidia kuonyesha treni iko wapi na kwa wakati gani njia nzima inapokua safarini na kwamba mfumo huo unaruhusu kuisimamisha treni sehemu yoyote kwa kutokea stesheni au makao makuu kwa kutumia mfumo wa kompyuta.

No comments:
Post a Comment