Kitendo hicho kimetokana na hali ya taaruki inayoendelea kutanda katika jamii za waisilamu na wakristo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo BBC imegundua mambo ya kutisha yanayofanyika mjini Bangui ambao ni mji mkuu wa taifa hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na BBC ilidai kuwa mwanaume huyo alifanya kitendo hicho kama hatua ya kulipiza kisasi baada ya wapiganaji wa kiislam kumuua mkewe aliyekuwa mjamzito na wifi yake pamoja na mwanawe.
Aidha mwanamume huyo kwa jina Ouandja Magloire alisema kuwa kila mtu ameghadbishwa na wapiganaji waisilamu na hakuna atakayewasamehe kwa walichokifanya.
Anasema alimuona mwathiriwa akiwa ameketi ndani ya basi moja. Alimtoa nje na kuanza kumshambulia na punde si punde akasaidiwa na umati uliokuwa unashuhudia kitendo hicho ambao pia ulimshambulia mwathiriwa huyo.
No comments:
Post a Comment