Taarifa
tulizozipokea kuhusu ajali iliyotokea tarehe 01/01/2014 na kusababisha kifo cha
mtu mmoja ilitokea mkoani Morogoro eneo la Kidoma, Mikumi, saa tisa alasiri
katika barabara ya Iringa/Morogoro wilayani Kilosa.
Ajali
hiyo ilisababishwa na basi la TAQWA lililokuwa kwenye mwendo kasi na kukutana
na scania ya mizigo. Pamoja na kifo cha mtu mmoja, ajali hiyo ilisababisha
majeruhi 15.
Basi
aina ya Nissan la kampuni ya TAQWA lenye usajili T776CRN, lilikuwa linaendeshwa
na dereva Bw. Hamad Baro, lilikuwa linatoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam.
Wakati
gari la mizigo aina ya Scania yenye usajili T220BTG na tela T220BTG likitokea
Harare, Zimbabwe kuelekea Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment