Thursday, December 26, 2013

MEGATRADE YATOA MISAADA KWA WATOTO

Arusha

KAMPUNI ya Megatrade Ivestment kupitia kinywaji chake cha K-vant Gin imetoa misaada ya vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwaajili ya sikukuu ya krismasi na mwaka mpya katika kituo cha New Paradise kilichopo kata ya sokoni 1 jijini Arusha

Akikabidhi msaada huo juzi kituoni hapo Meneja mauzo na masoko Goodluck Kway wa kampuni ya hiyo kupitia kinywaji chake cha K-vant Gin alisema utowaji wa misaada kwa makundi maalum yenye uhitaji ni utaratibu wao wa kurudisha faida waliopata kwa mwaka mzima kwa jamii

Alisema msaada huo umeweza kugharimu kiasi cha shilingili Milioni moja ambapo watoto hao wataweza kusherehekea sikukuu kama watoto wengine huku akitoa rai kwa makampuni kujitokeza kuwasadia watu wenye uhitaji

Misaada iliyokabidhiwa kituni hapo ni pamoja na sukari,mafuta ya kula,mchele,katoni za soda,sabuni,kalamu,madaftari,unga wa ugali,unga wa nganao na maziwa

Mlezi mkuu wa kituo hicho Christopher Kaaya alisema kampuni hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao na amewaomba waendelee na moyo huo wa kuwasaidia

“Mungu awazidishie sana kwa sababu wamekuwa watu wa karibu kwetu hata siku ya kwanza walituchangia katika ujenzi wa jengo hili na pia kila mwaka lazima watuletee zawadi za chrismasi na mwaka mpya”alisema Kaaya

Kituo hicho kinajumla ya watoto 24 wasichana wakiwa 14 na wavulana 10 ambapo idadi imeongezeka ukilinganisha na mwaka jana watoto walikuwa 20 tu kituoni hapo

No comments:

Post a Comment