Sunday, December 29, 2013

MAJANGA: WAGANGA WA KIENYEJI WAITABIRIA CCM

MWANZA

Makamu  wa Rais Mtendaji wa Chama cha Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala,Tanzania Traditonal Treatment Organazation (TATETO), Dkt Swalehe Issa Bukukwe,amekitabiria Chama cha Mapinduzi (CCM) akisema, kitaanguka kwenye uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kinyume na alivyotabiri awali.

Kwamba utabiri wake wa Oktoba 2 mwaka 2011,ulionyesha CCM chama ambacho kinaongozwa na nyota ya darala la juu ya Simba, kingeshinda kwenye uchaguzi huo kutokana na nyota yake kung’ara,lakini utabiri huo umegeuka.

Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili juzi ofisini kwake Mabatini,Mwanza, Dkt Bukukwe alisema ,CCM mwaka 2015 itaanguka kwa sababu mbalimbali zikiwemo ukiukwaji wa maadili na viongozi waliopewa dhamana kushindwa kuwajibika kwa wananchi.


Dkt Bukukwe alisema kuwa utabiri huo unaonyesha mfumo chama alichokitabiria ushindi, upo kinyume na viongozi waliopewa dhamana na Rais Jakaya Kikwete.Pia chama kiko mikononi mwa maatajiri wachache,hakiko kwa wananchi hali ambayo imekatisha tamaa.

Alisema CCM itaanguka kwa kuwa tayari viongozi na watendaji wenyewe wana utayari wa chama chao kushindwa kwenye uchaguzi huo,ndiyo maana wanashindwa kusimamia sera na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama chao na kushindwa kuwajibika kwa wananchi .

“Utabiri wangu hautoki patupu ni wa uhakika.Vyanzo vya utabiri vinaonyesha CCM itaanguka,waliopewa dhamana ya madaraka na JK hawamsaidii,hawazingatii miiko ya uongozi na hawawajibiki kwa wananchi,ambapo vitendo vya rushwa,ubadhirifu na ufisadi vimekithiri,hali ambayo imewakatisha tamaa wananchi na vinawezakuwa turufu ya kukiangusha chama hicho, ”alisema Dkt Bukukwe.

“Ninataka nikamwone JK Ikulu na kupitia vyombo vya habari,aniruhusu nikamtabirie hayo maana utabiri huo, unaonyesha kushindwa kwa CCM na aanguko lake ni nini na kwa nini imekuwa hivyo.Ni utabiri unaoambatana na tiba au utatuzi wa matatizo ya chama na serikali yake. ”

“Hili napaswa nimweleze JK badala ya kuyasema sasa na nitamwelekeza,sababu CCM ikianguka yeye atakuwa wa kwanza kuuwajibika ingawa nafahamu upo mkakati mrefu wa kukijenga chama upya katika mfumo wa kuwajibika kwa wananchi.Lazima kuwe na mabadiliko katika nafasi za juu hadi chini ili wananchi wafahamu chama chao kipo.” Alisema Dkt Bukukwe

Kwamba viongozi wa CCM chini ya JK si mzuri na hauridhishi, ni mzigo usiobebeka mwaka 2015 na hauna sababu ya kuwapo pale katika ngazi ya Taifa hadi matawi,hali inayotishia anguko kwenye uchaguzi huo wa mwaka 2015, kinyume cha utabiri ulivyo.

“Mwenyekiti wa CCM Taifa,haelewi ama hafamu tafsiri ya nyota inayokiongoza chama chake.Mimi kama Dkt wa kinajimu hajanipa fedha.Utabiri wangu wa Oktoba 2, 2011 nilitabiri CCM itashinda 2015 dhidi ya CUF na CHADEMA.”Alisema Dkt Bukukwe na kuongeza;

“Lakini CHADEMA ingeweza kuweka ushindani mkubwa na kupata matokeo mazuri yaa kuunda serikali ya mseto,ila tofauti yao ilikuwa ni daraja moja.Ingepata uwakilishi katika serikali ya mseto kwa viti vya ubunge, nafasi ya Waziri Mkuu na Mawaziri.Nyota ya CHADEMA ni mwezi.CUF wao nyota yao ni Nge,wange gawana viti kuunda serikali .”

Dkt Bukukwe aliwahi kutabiri Rais Kikwete, kushinda uchaguzi Mkuu mwaka 2010 akashinda na alirerejea tena kutabiri ushindi wa Dkt Dalali Kafumu, utabiri ambao ulidhihirika baada ya kushinda katika uchaguzi mdogo wa Igunga mwaka.

Maelzo ya Picha


Pics 1.Dkt Swalehe Issa Bukukwe,akisistiza kuwa CCM itaanguka kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 wananchi watakapotumia kura yao vizuri ,kwa sababu kero zao nyingi hazijatatuliwa.



No comments:

Post a Comment