TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Taasisi mbali mbali za kijamii, vyama vya
kitaaluma na vyama vya siasa vipatavyo 50 hadi leo, Jumanne, Desemba 31, 2013, vimewasilisha
majina ya watu wao ambao vinapendekezwa wafiriwe katika kuteuliwa kuwa Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba.
Taarifa iliyotolewa leo mjini Dar Es Salaam na
Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa taasisi hizo
zimewasilisha majina yao kwa mujibu wa mwaliko uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa makundi yaliyobainishwa
katika Kifungu cha 22(1) (c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (Sura ya 83).
Taarifa hiyo imesema kuwa makundi hayo 50
yaliyowasilisha majina yanayopendekezwa kwa ajili ya uteuzi yanatokana na barua
169 zilizopokelewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue na Ofisi ya
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar.
Makundi ambayo yamewasilisha majina ni
yafuatayo: Shirika la Wasaidizi wa Jamii
Kabila la Wagogo, Tanzania Association of Social Workers (TASOWA), Teachers and
Student Forum Tanzania, Tanzania Women Teachers Association, Umoja wa Wanawake
Wajane Wilaya ya Karagwe na Kyerwa (UWK), Tanzania Peace and Development
Society, Better World Organization (BWO), Youth Focus and Development, Association
of Traditional Medicine Man, Registered Centre for Good Governance and
Development in Tanzania, Chama Cha Kijamii (CCK), CHANETA na Muungano wa
Wanajeshi Wastaafu Tanzania.
Makundi
mengine ni Legal Aid Iringa Village, Tanzania Kilolo Orphans and Social
Development Organization, Legal aid and Social Welfare Association, Legal and
Human Right Centre, Tanzania Lift Initiative NGO, Kilolo Paralegal Unit, Women
Development and Social Activities Association, Defence of Human Right/Citizen
Rights, DAWSEN Trust Fund, Baruti Development Association (BADEA), Living Hope
Ministries Trust, EFATHA Ministry, Bethel Assemblies of God Tanzania, Muslim
and Christian Brotherhood Society, Baraza Kuu la Waislamu wa Kondoa – Tanzania
na Jesus Temple Inner Transformation News.
Taasisi
nyingine ni Jumuiya ya Waithna Asharriyyah Tanzania, Rehmatfi Sabilillah Trust of Tanzania, Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), National
Reconstruction Alliance (NRA), Sauti ya Umma (SAU), Chama cha Demokrasia
Makini, African Progressive Part – APPT Maendeleo, National League for
Democracy, Tanzania Film Federation, Taasisi ya Maendeleo ya Utamaduni, Al-Amoud
General Enterprises, Blue Belt and Water Sources Control, Community Development
Training Institute – Tengeru, Tanzania
Medical Student Association, Tanzania Sea Farmers Union, Medical Association of
Tanzania, Chama cha Wastaafu wa Mbinga, Union of Tanzania Press Clubs, Umoja wa
Wanawake Tanzania, Alliance for Tanzania Farmers Party, Tanzania Social
Economic and Environment and Wellbeing.
Kwa vile mwisho wa kupokea orodha ya majina hayo
ni tarehe 02 Januari, 2014, Balozi Sefue ametoa mwito kwa makundi mengine
ambayo hayajawasilisha orodha hiyo kufanya hivyo kabla muda uliowekwa kuisha.
Aidha, wakati wa kuwasilisha ni muhimu kuzingatia vigezo vilivyowekwa na sheria
na kama vilivyofafanuliwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 443 lililochapishwa
tarehe 13 Desemba, 2013. Vilevile ni muhimu kuzingatia kuwa majina
yanayopendekezwa na Taasisi au makundi yaliyoainishwa kwenye sheria na siyo mtu
binafsi kujipendekeza mwenyewe.
Kwa
wale watakaojipendekeza wenyewe wajue kuwa watakuwa wanakwenda kinyuma na
maelekezo.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31
Desemba, 2013
No comments:
Post a Comment