Monday, July 15, 2013
WAFUNGWA MARUFUKU KUONANA NA WAANDISHI WA HABARI
Wakati serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuweka wazi kuwa wafungwa wako huru kuzungumza na waandishi wa habari, kwa upande wa Jeshi la Magereza nchini limesema wafungwa hawaruhusiwi kisheria kuzungumza na waandishi wa habari, isipokuwa wanahaki ya kupata taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari kama vile magazeti redio pamoja na tv kwa kuwa hiyo ni haki ya kila mtu.
Kauli hiyo ilitolewa na msemaji wa Jeshi la Magereza Kamishna Mwandamizi Msaidizi. Omari Mtiga, alipokuwa akizungumza na waandishi ofisini kwake, aliweka wazi kuwa kupitia sheria namba 34 ya mwaka 1967 wafungwa hawaruhusiwi kuongea na waandishi wa habari isipokuwa wanahaki ya kupata taarifa.
Alisema vyombo hivyo ndivyo hutumika kufikisha taarifa za habari kwa wafungwa, lakini hawatakiwi kuzungumza na vyombo vya habari.
Ufafanuzi huo ulitolewa na kamishna huyo ili kueleza kama wafungwa upande wa bara wanaruhusiwa kuzungumza na waandishi wa habari kama ilivyo kwa wenzao wa Zanzibar.
Huko Zanzibar Waziri wa nchi Ofisi ya Rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi , Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini, alisema kuwa wafungwa na mahabusu wapo huru kuzungumza na vyombo vya habari , kwani fursa hiyo ipo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment