Monday, July 15, 2013

PIGO, WANAJESHI 7 WAUWAWA DARFUR


Wanajeshi 7 kati ya 36 wameuwa Darfur, mauaji wa wanajeshi 7 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliokuwa wanalinda amani Darfur, Sudan wauwaa baada ya kushambuliwa na waasi wa Sudani.

Mbali na vifo hivyo askari wengine 14 wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi la kushtukiza lililofanyika na kundi la waasi.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, msemaji wa jeshi hilo Kanali Kapambala Mgawe, alisema wanajeshi hao walivamiwa wakati wakiwa kwenye msafara wa kuwasindikiza waangalizi wa amani ambao walikuwa wanatoka eneo la Khor Abeche kwenda Nyara Darfur.

Aliweka wazi kuwa kifungu namba 6 cha majeshi ya kulinda amani kinakataza matumizi ya nguvu lakini kutokana na hali hiyo iliyojitokeza JWTZ inaangalia mpango wa kufanya mazungumzo na UN ili kuangalia kama wanaweza kutumia kifungu cha 7 ambacho kinaruhusu matumizi ya nguvu hasa wakati wa kujiami.

JK ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana, ilisema rais kikwete anaungana na watanzania wote na hasa maofisa na wapiganaji wa JWTZ na familia za wafiwa kuomboleza vifo hivyo.





No comments:

Post a Comment