Wednesday, July 17, 2013

ROONEY ASHIKWA NA HASIRA , ACHANGANYIKIWA'



Wayne Rooney kashikwa na hasira huku akiwa amechanganyikiwa kuhusu nafasi yake katika timu yake ya muda mrefu, Manchester United, baada ya Meneja David Moyes kusema mshambuliaji huyo sio chaguo lake la kwanza nyumbani Old Trafford.

Rooney, 27 ameeleza kuvunjika moyo kwa wakuu wa klabu hiyo na kusisitiza hatokubali kuwa msaidizi wa Robin van Persie.

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza amebakiza miaka miwili kabla ya kumaliza mkataba wake akiwa Man U. Amekua akifuatiliwa sana na wapinzani wa Man U katika ligi ya Premier, Chelsea na Arsenal.
Magoli ya Rooney kwenye Ligi ya Premier

2002-03: sita
2003-04: tisa
2004-05: 11
2005-06: 16
2006-07: 14
2007-08: 12
2008-09: 12
2009-10: 26
2010-11: 11
2011-12: 27
2012-13: 12
Total: 156

Moyes, alikaririwa jumapili katika gazeti akirudia kusema Rooney hauzwi “ana nafasi kubwa sana ya kucheza”, hayo aliyasema wakiwa Bangkok wiki iliyopita 

Lakini Wayne Rooney alikasirika Meneja wake alipoongeza kwamba “kwa ujumla nafikiri tunamuhitaji sana Wayne kama Robin van Persie akiumia. Nahitaji fursa nyingi iwezekanavyo”


Rooney anaamini hana jipya United baada ya misimu 9 ya mafanikio katika klabu hiyo na ameshafanya maongezi kabla ya kurudi kutoka kwenye ziara Australia pamoja na Mashariki ya Mbali akiwa na majeraha ya mkono.

Akiwa ameachwa benchi katika mechi kadhaa muhimu na kocha wa zamani Sir Alex Ferguson msimu uliopita, alieleza nia yake ya kuondoka United, lakini vyanzo vilivyoko karibu naye vinasema hajatoa maombi yoyote mpaka sasa.

 Timu ya Chelsea kupita Meneja wake Jose Mourinho ilionyesha kumhitaji Rooney wakati anahojiwa na BBC jumanne iliyopita na kwamba wanafuatilia kwa karibu kinachoendelea Man U

Ziara ya Man Utd
  • 13 July Singha All Stars (Bangkok) - Lost 1-0
  • 20 July A-League All Stars (Sydney)
  • 23 July Yokohama F Marinos (Yokohama)
  • 26 July Cerezo Osaka (Osaka)
  • 29 July Kitchee FC (Hong Kong)
Mourinho anaamini Rooney kukosa kucheza kwa muda mrefu italeta matatizo kwa timu ya Taifa ya Uingereza na Meneja wake Roy Hodgson kabla ya kufika mwakani katika mashindano ya kombe la dunia Brazil. 

"Kama Wayne ni chaguo la pili Manchester United, basi timu ya taifa itaadhirika," alisema Mourinho. 

Uongozi wa juu wa United umepanga kumuangalia kwa karibu mshambuliaji huyo katika msimu huu kabla ya kufanya maamuzi kwaajili ya baadae. 

Lakini Rooney amekosa raha sana kutokana ujumbe alioupata kutoka katika klabu hiyo ya Old Trafford, jambo ambalo litafahamika wiki chache zijazo

Woodward anatarajiwa kurejea nyumbani baada ya kuudhuria mechi iliyochezwa jumamosi dhidi ya A-League All Stars ya Sydney Australia katika uwanja wa ANZ, lakini Moyes atachelewa kurudi Uingereza kwa wiki moja zaidi kwani United wanamechi nyingine Japan na Hong Kong kabla ya ziara yao kuisha.


Wakuu wa United hawakuweza kupatikana kuongelea jambo hilo.


No comments:

Post a Comment