Serikali ya Kenya imepeana idhini ya kuanza kwa uchimbaji wa madini ya niobium katika eneo Kwale.
Kampuni ambayo itaendesha uchimbaji wa madini hayo ya Cortec Mining Kenya imetangaza kuwa mamlaka ya kitaifa ya kutunza mazingira – Nema imepeana kibali kuruhusu uchimbaji huo.
Uchimbaji huu ukianza serikali itanufaika na mapato ya moja kwa moja ya shilingi bilioni 26.
Kampuni hii ambayo ilipewa kibali cha kuanza kuchimba madini hayo mnamo machi mwaka huu itaanza kufanya uchimbaji katika eneo la Mrima.
Eneo hili la Mrima limetajwa na wataalam wa madini kuwa na takriban tani mjazo 105 za madini haya ya Niobium, na uchimbaji wake unaweza kuendelea kwa kati ya miaka 15 na 20.
Ikiwa nchi ya Kenya ikianza uchimbaji wa madini haya itakuwa nchi ya sita kote Duniani katika uchimbaji wa madini haya.Kwa sasa nchi ya Brazil na Canada ndizo zinaongoza kwa uchimbaji wa Niobium.
Madini ya Niobium uchanganywa na aina tofauti ya vyuma ili kuzipatia nguvu na kupunguza uzito wake.

No comments:
Post a Comment