APPLE KUCHUNGUZA
Kampuni ya
Marekani ya Apple Inc inachunguza tuhuma za China kwamba mwanamke aliyekufa
baada ya kupigwa shoti ya umeme alipokuwa anajaribu kupiga simu kwa kutumia
Iphone5 wakati inachaji.
Ma Ailun, mfanyakazi
wa shirika la ndege la China Southern Airlines, alikuwa anapokea simu aliyopigiwa
alhamisi iliyopita ndipo inadaiwa alipopigwa shoti, polisi ilidai katika ripoti
yake ya jumapili.
Kwa mujibu
wa shirika la habari la China, Xinhua, wakati polisi wanaendelea na uchunguzi
wake, haijaweza haswa kudhibitisha sababu ya kifo hicho ni nini, kama ni simu
au kitu kingine.
Katika taarifa
iliyopokewa na shirika la habari la Marekani, CNN, Apple imesema “tumeguswa na
kusikitishwa sana kusikia taarifa hizi mbaya na kutuma rambirambi zetu kwa
familia ya Ma. Tutachunguza kwa undani na kutoa ushirikiano wa kutosha kuhusiana
na suala hilo”
Mijadala imekuwa
ikiendelea kwenye mitandao ya jamii haswa swali kubwa likiwa ni imekuwaje Mchina
huyo mwenye miaka 23 anaeishi Xinjiang jimbo la Uygur afe kwa simu.
"Natumaini kuwa Apple Inc. Itatoa maelezo. Pia nategemea wote mtaacha
kutumia simu zenu wakati ziko kwenye umeme zikiwa zinachaji " dada yake Ma
aliweka kwenye maelezo hayo kwenye mtandao wa kijamii wa Weibo, mtandao wa Kichina
unaofanana na Twitter kwa huduma zake.
Wakati huo
huo, baba yake Ma, Ma Guanghui, alisema mtoto wake alipigwa shoti na kuongeza
kuwa mwili wake unaonesha dalili zote za kupigwa shoti, Xinhua ilieleza
Lakini katika
ripoti ya jumatatu ya Xinhua ilidai kwamba simu za mkononi zina toa umeme
kidogo sana wenye volt 5, ambao hauwezi kuudhuru mwili wa mwanadamu.
No comments:
Post a Comment