Darubini ya
anga ya Hubble ya Nasa imegundua mwezi mpya unaozunguka sayari ya Neptune, Nasa
imedhibitisha habari hizo.
Kwa mujibu
wa habari za mtandao wa BBC kitengo cha sayansi na mazingira, mwezi huo uko
katika vipimo vya S/2004 N 1, huu ni mwezi wa 14 ulionekana ukizunguka sayari
hiyo kubwa. Mwezi huo pia unaonekana kuwa ni mwezi mdogo zaidi unaoizunguka
Neptune katika umbali wa kilomita 20 (maili 12), na mwezi huo unakamilisha
mzunguko wake kila baada ya saa 23.
Mwana anga
wa Kimarekani, Mark Showalter aliona kakitu kadogo kama nukta wakati
anachunguza ukanda unaozunguka sayari hiyo ya Neptune.
Nasa imedai
kuwa mwezi huo umefifia zaidi ya mara milioni 100 kuliko nyota inayoweza
kuonekana kwa jicho la kawaida. Ni kadogo sana kiasi kwamba chombo cha anga kilishindwa
kuuona mwezi huo mwaka 1989 wakati chombo hicho kinaizunguka sayari hiyo.
Bw Showalter
alitumia mbinu yake ya cheche nyeupe iliyokuwa ikitokea kila mara kwa zaidi ya
mara 150 na kisha piga picha kwa kutumia darubini ya Hubble kati ya mwaka 2004
na 2009.
Kwa mujibu
wa BBC Bw. Showalter alieleza “huo mwezi
unakenda haraka sana hivyo ilitulazimu kutafuta namna ya kufuatilia mwenendo
wake ili kupata maelezo ya kutosha ya mfumo huo”.
“ni njia ile
ile mpigapicha anayotumia kumpiga picha mkimbia anayekwenda kwa kasi ambapo
mkimbiaji anaendelea kuonekana wakati nyuma yake panakuwa hapaeleweki” alimaliza
No comments:
Post a Comment