Mtu asiyejulikana amegongwa na treni na kufa katika reli ya TAZARA katika mji wa Mbeya eneo la Darajani saa tano asubuhi jana. Mwili (pichani) wa mtu huyo ambaye jina lake halikutambulika mara moja, ulikutwa bado katika eneo hilo la reli saa nane mchana ambapo inadaiwa aligongwa na taarifa kutolewa polisi lakini mwili haukuwa umetolewa mpaka muda huo. (picha na ImmaMatukio Staff)
No comments:
Post a Comment