Wednesday, June 05, 2013

SAMSUNG YAIBWAGA iPHONE MAHAKAMANI




Kamisheni ya kimataifa ya biashara ya Marekani (ITC) jana ilitupilia mbali malalamiko ya  kampuni maarufu ya Silicon Valley (Apple) kwamba iliingiliwa na wamiliki wa Samsung katika hatimiliki ya uwezo wa bidhaa zake kusafirisha huduma mbalimbali kwa
wakati mmoja na kwa ufasaha kwa kutumia teknolojia ya 3G.

Tume huru ilitupilia mbali ombi la kuzuia kuingiza na kuuza simu zinazofanan na iPhone4, iphone 3GS, iPad 3G pamoja na iPad 2 3G kusambazwa na kampuni ya AT&T, ambao ni wauzaji wakubwa wa bidhaa za Apple nchini Marekani wakati Samsung ikifungua mashtaka mwaka 2011.

Wakati bidhaa hizo zinazounganishwa bara la Asia ambapo inatarajiwa kuwa Rais wa Marekani Barack Obama ndani ya siku 60 atapitia na kufanya maamuzi ya kesi hiyo. Na kama hatosema chochote basi utekelezaji wa maamuzi hayo utaanza mara moja.

Haijajulikana mara moja madhara ya uamuzi huo kwa kampuni ya Apple au AT&T kama Rais Obama atakaa kimya na kuruhusu uamuzi uendelee, wakati uamuzi wake utakuwa ni mwisho wa urefushwaji wa kesi hiyo.

Wakati bidhaa hizo zina zaidi ya mwaka mmoja, baadhi kama iPhone4 bado inafanya vizuri sana sokoni.

Katika makubaliano ambayo ITC inayatambua bidhaa mpya kabisa kutajwa ni iPhone4 ambapo tayari ilishaingia sokoni na kusaini makubaliano na makampuni makubwa mbalimbali kama vile Verizon Wireless, ambapo haitoadhirika na maamuzi hayo.

iPhone 4 yaweza kuondolewa kabisa katika kipindi cha mwaka mmoja ujao kama Apple itaendelea na mipango yake na kuendelea na toleo lake la iPhone5 kitu ambacho ni matarajio ya makampuni mengi ulimwenguni.

Lakini hata kama msimamo wa kuingiza bidhaa za Samsung Marekani ukiendelea, idara ya mapato ya Marekani itaendelea kuchelewesha bidhaa nyingine za Apple, kwa mujibu wa Susan Kohn Ross, ambaye ni mshirika katika ofisi ya Mitchell Silberberg & Knupp.

‘Hii italeta mtikisiko mkubwa kwa Apple’ alisema Mitchell ‘Idara ya mapato ina kazi ngumu sana, inabidi wakague kila mzigo unaoingia’

Simu ya iPhone inaingiza zaidi ya nusu ya faida ya kampuni ya Apple.

Wakati kampuni hiyo haiweki wazi mauzo ya simu zake au hata modeli nyingine za iPad, pamoja na toleo lake jipya la iPhone ambapo ni zaidi ya iPhone milioni 100 zinauzwa kwa mwaka.


No comments:

Post a Comment