Saturday, June 15, 2013

BREAKING NEWS: TAARIFA ZINAZOENDELA KUINGIA TOKA ARUSHA HALI NI MBAYA SANA



Hali ilvyo hospitali ya Seliani, Arusha

Habari zinazoeendela kuingia kutoka Hospitali ya Seliani iliyoko mjini Arusha, hali mbaya sana watu wanataharuki, vilio vimetawala kila kona ya hospitali hiyo, inasemekana majeruhi ni wengi sana na ni zaidi ya 70, hali ya majeruhi wengi ni mbaya sana wakati wengine ni taabani, wakiwa katika maumivu makubwa.


Watu wengi wamejitokoza katika hospital hiyo, makamanda wa CHADEMA wakiwa na askari wa zimamoto wanasaidiana na madaktari kuhudumia na kutoa huduma ya kwanza.

Inadaiwa mtoto ambaye hakuweza kutambulika mara moja yuko mahututi na kudiwa kukaribia kufariki.

Kamanda wa mkoa wa Arusha Liberatus Sabas yuko hospitali hapo kushuhudia hali ilivyo. Kamanda Huyo bado hajatoa taarifa yoyote mapaka tunaendelea kukupa taarifa hizi

Mt meru

Na katika hospitali ya Mount Meru, mkoani Arusha inadaiwa kuna majeruhi zaidi ya 20 na hali zao pia ni mbaya.

Hali ya waandishi

Mwandishi wetu aliyeko eneo la tukio anatupasha habari hizo katika mazingira magumu sana kwani waandishi hawapewi ushirikiano wakutosha. Mwandishi huyo amenyang’anywa kamera yake baada ya kupiga picha hata baada ya kujitambulisha.


No comments:

Post a Comment