Friday, June 14, 2013
BREAKING NEWS: KWANINI OBAMA HAENDI MIKUMI
Taarifa zilizotufikia hivi punde zimeeleza kutokuwepo kwa ziara ya Obama nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoandikwa na kuchapishwa na gazeti la kila siku la Washington Post la jana alhamisi zinasema ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama aliyekuwa anafuatana na mkewe Michelle kutembelea
Tanzania imefutwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa AP, inadaiwa taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti la Washington Post zimetokana na kabrasha za mipango ya usalama iliyovuja.
Kwa mujibu wa kabrasha hizo zimedai kuwa Rais Obama ambaye alikuwa anakuja Tanzania mwishoni mwa mwezi juni, ziara hiyo imefutwa kutokana na gharama kubwa za ulinzi mkali kupita kiasi.
“Safari hiyo ingehitaji timu kubwa sana ya walinzi huku wakibeba bunduki zenye uwezo mkubwa sana ambao ungeweza kuua duma, simba na wanyama wengine ambao wangetishia usalama” iliandika ripoti hiyo.
Kabrasha hiyo ilitolewa na mtu aliyeguswa na gharama zitakazotumika katika safari nzima katika mpango mzima wa usalama kuanzia Senegal, Tanzania na Afrika Kusini,
Ripoti hiyo haikutoa maelezo yoyote kuhusiana na gharama.
Gazeti hilo lilieleza kuwa Ikulu ya White House imefuta safari hiyo jumatano wiki hii baada ya kabrasha hilo kuuliza ‘lengo la gharama hizo’. Obama na mkewe wangekwenda kukaa zaidi ya masaa mawili katika mbuga ya Taifa ya Mikumi
Hata hivyo Ikulu ya White House haikuweza kupatikana mara moja kuzungumzia suala hilo, lakini msemaji alidai kuwa safari ya Afrika Kusini kwenda kisiwa cha Robben ilipo jela aliyowahi kufungwa Rais Neslon Mandela itaendelea.
“Hatuna uwezo wa kugharamia ujumbe wa safari ya Rais, na kipaumbele ni kutembelea kisiwa cha Robben, kwa hayo masaa mawili ya Tanzania” alisema msemaji huyo Josh Earnest
“Kwa kweli hatuwezi yote mawili” Alisisitiza
Washington Post ilieleza ziara ya Obama kuja Afrika ni ya kwanza toka aingie ofisini Januari 2009 na ingegharimu serikali ya Marekani kati ya dola za milioni 60 mpaka 100, kutokana na makadirio ya gharama za safari hiyo kwa sasa.
Mamia ya wanausalama wa Marekani wataondolewa katika ziara hiyo, ambapo ni pamoja na ndege za kijeshi, meli kubwa za usalama zenye vituo vikubwa vya afya baharini ilisema ripoti hiyo.
Magari chungumzima yasiyopenyeza risasi (bullet proof) kwenye vioo vyake ikiwa ni pamoja na vioo vikubwa kwaajili ya hoteli ambayo Obama angefikia yalikuwa yaingizwe kwa ndege kubwa za kijeshi katika nchi hizo tatu ambazo Obama angetembelea
“Ndege za kivita zingeruka kwa zamu kulinda anga ambayo rais atakuwepo” gazeti hilo liliripoti taarifa hizo za idara ya usalama.
http://www.newvision.co.ug/news/643933-white-house-cancels-obama-safari-in-tanzania.html
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Wacha uongo wewe,jaribu kusoma kwanza habari yenyewe ndo uje kuhabarisha watu hapa jamvini kwako, acha uvivu wa kusoma ili upate haabari na kuandika vitu vyenye ukweli hapa kha
ReplyDeleteKweli kabisa tunakubali kughafilika, asante kwa kuliona na kushauri, tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kutotoa taarifa sisizo na ukweli. Samahani tena kwa usumbufu tuliosababisha. Asante
ReplyDelete