Aliyekuwa
Waziri Mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi amehukumiwa kwenda jela miaka 7 na
kuzuiwa kuingia katika ofisi zozote za serekali baada ya kupatikana na kosa la
kufanya ngono na watoto wadogo.
Kwa mujibu
wa BBC, Berlusconi anaendelea kuwa huru baada ya kukata rufaa dhidi ya mahakama
ya Milan.
Washtakiwa
wote wawili mmoja akiwa ni tajiri wa vyombo vya habari, Bw Berlusconi na
msichana wa Moroco, Karima El Mahroug wamekataa kuwa waliwahi kukutana kingono.
“Ntapinga
hukumu yangu kwasababu sina kosa lolote” alieleza Bw. Berlusconi baada ya
hukumu kutolewa
Lakni Bw.
Berlusconi bado amezungukwa na kesi nyingie ambapo mwezi oktoba 2012
alihukumiwa kwenda jela kwa miaka 4 kwa kosa la kukwepa kodi, ambapo pia
alikata rufaa.
No comments:
Post a Comment