Amerudi China kama balozi wa soka wa taifa
David Beckham amerudi nchini China kwa kipindi cha wiki moja akiwa kama balozi wa kwanza wa soka nchini humo.
Kwa mujibu wa mtandao wa Sky News,
ikiripoti dakika chache zilizopita, katika safari hiyo, viongozi wa Kichina wanaamini kuwa Beckham atainua hadhi ya mpira nchini humo, kutokana na mechi kadhaa zilizochafua mchezo huo nchini China.
Beckham aliyekuwa nyota wa mpira katika timu ya taifa ya England na Manchester United ataenda China na kutembelea miji minne ya Hangzhou, Beijing, Shanghai na Nanjing pamoja na kutembelea vilabu mbali mbali vya soka nchini humo.
Safari yake ya kwanza katika nchi hiyo, Beckham aliyoenda kikazi katika ligi baada tu ya kumaliza na kujiuzulu akiwa katika klabu ya Paris Saint-German, Beckham alichangia fulana za mpira ili kusaidia kuchangisha fedha kwaajili ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Ziara ya Beckham inafanyika katika kipindi kibaya sana cha soka nchini China, ambapo timu ya taifa ya China imepoteza michezo mitatu katika mechi za kirafiki, ikiwa ni pamoja na mechi iliyocheza na Thailand jumamosi iliyopita.
No comments:
Post a Comment