Alikuwa anajibu swali aliloulizwa na
Wakenya, kuhusu ahadi ya kutembela nchi ya Kenya mahali alipozaliwa baba yake
mzazi katika kipindi chake cha urais. Alikuwa anaongea na mamia ya vijana
waliokutana nae Soweto, Chuo Kikuu cha Johannesburg leo.
“Bado
ntakuwa Rais kwa miaka mingine mitatu na nusu” alijibu alipoulizwa kwa kutumia
video ya kwenye mtandao kutoka Nairobi kwanini hatotembelea Kenya.
“Unagundua
kama Rais watu sio tu wanataka utekeleza ahadi zako lakini wanataka utekeleze
ahadi zao jana” alisema Obama alipokuwa anajibu swali hilo.
Lakini Obama alikubali kwamba maamuzi ya
mahakama ya kimataifa ya ICC yamechangia maamuzi yake ya kutokwenda
Kenya
“Sidhani kama ulikuwa wakati muafaka mimi kutembelea
nchi hiyo” alisema huku akiendelea kusisitiza kwamba bado ana mpango wa kwenda
Kenya kabla muda wake wa urais haujaisha, ambapo itakuwa mwaka 2017
Mapema katika mkutano na vyombo vya habari
akiwa mjini Pretoria, alisema kuwa ameiruka Kenya katika ziara yake kutokana na
migogoro, ambapo ICC inamshtaki Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa makosa ya
uhaini, yanayo husu mauaji, ubakaji, unyanyasaji na unyama ambayo yaliyofanywa
na wafuasi wake katika fujo za uchaguzi wa Kenya wa mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment