Saturday, May 11, 2013

MKURUGENZI WA WHATSAPP MESSENGER ATOBOA SIRI


Sijui kama ni sahihi kusema Mkurugenzi wa Whatsapp, Jan Koum hapendi kuonekana au kujulikana. lakini huwa si muongeaji sana.Koum ndie mwanzilishi wa mtandao wa meseji za bure maarufu na unaokuja juu kwa kasi kuliko yote ulimwenguni ambao kwa sasa umefikisha zaidi ya watumiaji milioni 200 kwa mwezi, watumiaji wengi zaidi kupita
hata ule wa Twitter.

Lakini Whatsapp imekuwa ikikwepa sana kujulikana, imekwepa kukutana na waandishi wa habari, mikutano na imekuwa ikifanya mambo yake kwa msaada wa wafanyakazi 40 tu huko Marekani kutoka kwenye kaofisi kadogo tu, huko Calif.

Koum ameeleza sababu moja wapo ya kujificha na kutotaka matangazo kwa kueleza kuwa katika miaka 10 aliyofanya kazi na mtandao wa Yahoo amegundua na kuamini kuwa matangazo yanaharibu mahusiano baina ya kampuni na wateja wake. 'huduma kwa wateja itashuka tu, sababu utataka kutoa huduma zaidi kwa watangazaji' na hilo ni tatizo sugu zaidi kwenye makampuni ya simu'

'makampuni ya simu yanajijali zaidi kuliko kuliko wateja wao kiasi kwamba kutangaza huko sio jambo zuri sana'alijibu alipoulizwa kwanini huwa Whatsapp haijitangazi kwenye mitandao  ya simu ili kukua na kuongeza soko lake ikiwa ni pamoja na kujitanua katika huduma za alipokuwa akihojiwa katika mahojiano maalum na mtandao maaru wa D: Drive

No comments:

Post a Comment