Tuesday, May 14, 2013
GADNER ATAJA MAJINA YA WASANII WALIOUNGANA NA JAYDEE
MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Juma Kassimu 'Juma Nature' ameungana na msanii wa kike wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura 'Lady Jaydee' katika uzinduzi wa albamu yake ya sita iitwayo 'Nothing But The Truth' itakayozinduliwa Juni 31 mwaka huu.
Wasanii wengine ambao wameungana na msanii huyo ni pamoja na msanii nguli wa muziki wa Hip Hop Professa Jay, TID na Grace Matata .
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Gadner G. Habash ambaye ni Meneja na Mume wa Mwanamuziki huyo alisema kuwa Juma Nature ni miongoni mwa wasanii ambao ameamua kuungana na Jidee kuwepo katika uzinduzi huo.
Alisema kuungana kwake kumeongeza nguvu katika uzinduzi huo ambao utakuwa ni wa aina yake.
Alisema kuwa uzinduzi huo ambao unatarajia kuanza mapema utaenda sambamba na mashabiki wake kula chakula cha jioni.
"Uzinduzi huu utakuwa ni wa kipekee sana na utafanyika Nyumbani Lough nje pale kwenye park ya magari patatengenezwa kimataifa hivyo patatosha na mashabiki wa Jidee watapata burudani ambayo wanaitarajia " alisema Gadner
Akizungumzia kuhusu swala la kesi inayomkabili msanii wake ambapo anatakiwa Mahakamani Mei 27 kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili huku zikiwa zimebaki siku 4 kufanya uzinduzi wake.
Alisema Mahakamani ni sehemu ya kusikiliza na kufanya maamuzi na si kuharibu mipango ya watu hivyo anaamini uzinduzi wake hautoathirika.
"Tumejipanga vyema kwa ajili ya kukabiliana na kesi hiyo na mipango yetu inaenda vyema kwa ajili ya uzinduzi huo hivyo kila kitu kinaenda vyema" alisema Gadner.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment