Tuesday, May 14, 2013

ANGELINA JOLIE AONDOA MATITI


BAADA ya kugundulika kuwa yupo katika hatari ya ya kupata saratani ya matiti mcheza filamu mashuhuri duniani Angelina Jolie (37) ameamua kufanya upasuaji wa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wa uzazi.



Angelina ambaye ni mama wa watoto sita, alipoteza mamake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti.
Hayo alisema kwenye taarifa aliyoandika kwenye gazeti la New York Times, Bi Jolie alisema alifanyiwa uchunguzi wa celi zake na kugunduliwa kwamba alikuwa katika hatari ya kupata saratani ya matiti ndipo akaamua kukatwa matiti yake mawili.

Kulingana na taarifa ya Jolie alisema kuwa madaktari walitoa taarifa kuwa uwezekano wake kupata Saratani ya matiti ni asilimia 87 huku akiwa na asilimia 50 uwezo wake wa kuugua Sarati ya mfuko wa uzazi




No comments:

Post a Comment