Habari toka vynzo mbalimbali :
Leo kulikuwa na uzinduzi wa Parokia mpya ya Olasit mjini Arusha. Mgeni rasmi alikuwa Mwakilishi wa Papa toka Vatican. Kulikuwa na wageni wengi waliambatana na mwakilishi wa papa, wakiwemo maaskofu, mapadre na watawa kutoka mataifa mbalimbali.
Inasemekana walionekana watu waliokuwa kwenye mini bus wakirusha kitu kuelekea kwenye kanisa hilo wakati ibada inaendelea.
Taarifa zinaeleza kuwa eneo kubwa limetapakaa damu, watu wengi wamejeruhiwa. Inasadikiwa kuwa wapo waliokufa lakini haijathibitika. Muda huu vyombo vyote vya usalama vipo eneo la tukio.
email toka kwa mdau wa immamatukio
----------------
Mlipuko mkubwa umetokea katika kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasisi Arusha. Watu kadhaa wamejeruhiwa wakati wa ibada ya uzinduzi wa kanisa hilo iliyokuwa ikiongozwa na Balozi wa Papa nchini. Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi.
Source : ITV
----------------
Hali inakuwa tete katika nchi yetu Kanisani Parokia ya Olasit kumetokea mlipuko haijajulikana kama ni bomu au la ila watu wamejruhiwa inasikitisha.
Source: Radio Maria
Nukuu kutoka Redio Maria
....watu wengi wamejeruhiwa miguu
......ni mlipuko
.....Olasiti Arusha
...kitu kilirushwa au kutokea chini kwenye moramu iliyo mwagwa....
....kuna watu wanahisiwa kuja eneo la tukio kwa gari na kurusha hiko kitu na kukimbia kutokomea na gari...maelezo ya mtoto mdogo anaye sadikiwa kuona watuhumiwa....
...watoto wengi na kina mama wamejeruhiwa....
Kilikuwa ni kigango wakristo wakajichanga na kujenga kanisa kubwa na palikuwa na ugeni(balozi)kutoka Vatican alikuja kuzindua kama mgeni rasmi,majeruhi ni wengi ila vifo bado havijathibitishwa mpaka sasa hivi.Ni eneo la Olasiti kwa wakaazi wa Arusha au wanaoifahamu Arusha,radio Maria wanatoa taarifa kila mara.
.....mlipuko ulitokea katikati ya watu.....
....eneo limetapakaa damu....inasikitisha sana....
....niwakati Baba askofu akibariki maji ya baraka wakati anaweka chumvi ndani ya hayo maji (tendo la kubariki maji)..ghafra mlipuko ukatokea karikati ya watu....
....watu wako katika hali ya majonzi na masikitiko makubwa.....
source : Jamii forum
Huu ndio unyama na ndio dalili ya vita vya udini sasa, Eeh Mungu tuepushie mbali
ReplyDelete