Sir Alex Ferguson atastaafu umeneja na kufundisha
Manchester United mwisho wa msimu baada ya kuongoza klabu hiyo kwa misimu 26.
Ferguson mwenye umri wa miaka 71 ameiwezesha Man U kushinda jumla ya vikombe 38.
Kwa mujibu wa mtandao wa BBC,
inasemekana Sir
Ferguson ataendelea kuwa balozi na mmoja wa wakurugenzi wa Manchester United.
Katika ushindi wake ni pamoja na ushiriki wa
mara 13 katika ligi, mataji mawili ya ushindi, vikombe 5 vya kombe la FA pamoja
na vikombe 4 vya ligi.
‘Uamuzi wa kustaafu ni kati ya mambo
niliyofikiria kwa undani sana, na sasa ni muda muafaka’ alisema Ferguson
Jose Mourinho ametajwa kama mtu pekee anayeweza
kuchukua nafasi ya Sir Alex atakapoondoka. Pamoja na Jose, wengine wanaotajwa
ni pamoja na Meneja wa Everton, David Moyes, na Meneja wa Borussia Dortmund, Jurgen
Klopp.
‘Ni muhimu sana kwangu kuiacha klabu katika hali nzuri
iwezekanavyo na nnaamini nimeweza kufanya hivyo’ aliongeza Ferguson
‘kiwango cha timu hii ya ushindi, kiwango cha umri wa wachezaji,
maumbile ya wachezaji vitaendelea kuleta mafanikio katika kiwango cha juu zaidi
wakati muundo wa wachezaji chipukizi utaihakikishia timu ushindi wa fursa
nyingi zaidi za ushindi’ alimaliza
CHANZO : BBC SPORT
No comments:
Post a Comment