Wednesday, May 22, 2013

BREAKING NEWS: AJALI MBAYA YASABABISHA HASARA KUBWA


Lori la kampuni ya mafuta ya alizeti likiwa limebomoka vibaya na kusababisha mafuta kumwagika na kusambaa katika barabara ya Mandela na
Chan'gombe polisi jirani na kiwanda cha Serengeti Breweries, tukio hilo limetokea saa sita mchana leo.

Ajali hiyo imetokea wakati lori hilo likijaribu kuipita daladala na tela lake kuyumba na kuigonga daladala kwa nyuma na hatimae daladala kupinduka. Kwa muujibu wa taarifa tulizozipata mpaka sasa hakuna aliepoteza maisha.

Gari aina ya Toyota Prado nalo liligongwa na kusababisha kuharibika vibaya.

Blog ya matukio inaendelea kufuatilia ili kukujuza msomaji wetu. 





No comments:

Post a Comment