Monday, April 29, 2013

WANAFUNZI WA DSJ WAPATA AJALI, MMOJA APOTEZA MAISHA, CHANZO CHA AJALI CHABAINIKA

Hili ni gari lililopata ajali maeneo ya Chalinze mkoa wa Pwani jana usiku lenye namba za usajili T150 BJR Toyota Coaster ililokuwa limebeba wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari (DSJ) wakitokea katika ziara ya kimasomo mkoani Mbeya

Watu wawili akiwemo mwanachuo wa Chuo cha Uandishi wa Habari (DSJ) Deo Kibona amekufa na wengine 22 kujeruhiwa katika ajari ya gari walilokuwa wakisafiri kugongana uso kwa uso na lori la mafuta


Mwingine aliyekufa katika ajali hiyo ni Ally Kinyasi dereva wa gari lenye namba za usajili T 150 BJR Toyota Coaster ililokuwa limebeba wanafunzi wa chuo hicho cha DSJ wakitokea Mbeya katika ziara ya kimasomo

Kamanda wa Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Pwani Nassor Sisiwaya alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa gari lenye namba hiyo lililokuwa likitokea Mbeya liligongana uso kwa uso na lori la mafuta lililokuwa likitokea Dar es Salaam na kuelekea mikoani likiendeshwa na Mbwana Hassan

Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari namab T 151 baada ya kujalibu kulipita gari la mbele bila ya uangalifu na kusababisha gari lake kugongana uso kwa uso na lori hilo

No comments:

Post a Comment