MSANII wa muziki wa kizazi kipya anayeimba miondoko ya Hip Hop Farid Kubanga anayejulikana kwa jina la Fid Q yupo katika harakati za kumuenzi muimbaji nguli wa muziki wa taarabu Bi. Kidude kwa kuanzisha harakati za kujenga makumbusho nyumbani alipokuwa anaishi muimbaji huyo
Msanii huyo ameamua kumuenzi Bi. Kidude kwa njia ya kipekee kutokana na upekee alionao muimbaji huyo katika sekta ya muziki hali ambayo ilisababisha kutangaza nchini kupitia ziara ambazo alizokuwa akizifanya
Fid Q alisema kuwa kupitia nyimbo walioshirikiana inayojulikana kwa jina la 'Juhudi za wasiojiweza' ameamua kuingiza katika muito wa simu ambapo mapato yatakayopatikana yataingia katika ujenzi wa nyumba ya makumbusho ya Bi. Kidude
Alisema kuwa kutokana na aliyoyafanya mengi kulingana na umri wake anastahiri kujengewa nyumba ya makumbusho ambapo pia itaongeza ajira kwa vijana na kukuza kipato kwa nchi
"Bi. Kidude anastahili kujengewa makumbusho kwani hatu aliyokuwa amefikia hadi umauti umemkuta amekuwa ni muimbaji bora dunia kote kutokana na umri aliokuwa nao pamoja na uwezo wake kwenye uimbaji" alisema Fid Q
Pamoja na hayo Fid Q alitoa wito kwa yeyote yule ambaye ameguswa kwa ajili ya kuindeleza wazo lake la kujenga nyumba hiyo ya makumbusho kwa ajili ya kumuenzi muimbaji huyo kufanya hivyo kwa moyo na fursa ziko wazi
No comments:
Post a Comment