Friday, July 27, 2012

WATEJA WA VODACOM KUFURAHIA VIFURUSHI VYA CHEKA INTANET


Dar es Salaam 26th July, 2012…. Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imeanzisha vifurushi vipya vya Cheka intanet kwa bei nafuu. Ofa hiyo ambayo ni maalum kwa wateja wa malipo ya kabla inatarajiwa kuleta hamasa kubwa ya matumizi ya intanet kwa wateja kutumia simu zao kuperuzi na kupata taarifa mbalimbali.

Kwa kifurushi cha Cheka 200, mteja atapata dakika 15 za kupiga simu na SMS 15 kwa siku nzima, huku cheka 150 itampatia mteja dakika 5 na SMS 10, na kwa kifurushi cha Cheka 100 mteja atapata SMS 10 kwa siku. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Rene Meza, ofa hiyo imelenga kuwapa wateja kile wanachostahili. “Tukiwa tunapitia katika kipindi kigumu cha uchumi, tumeonelea kama Vodacom kutoa ofa ambayo itawawezesha wateja kuwasiliana na kupata taarifa kutoka sehemu mbalimbali kwa gharama nafuu. Ninawahimiza watanzania wote kutumia ofa hii,” alisema Meza.

Ofa hii imekuja wakati ambapo Vodacom Tanzania imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 120 katika kuboresha huduma na miundombinu ya mtandao mwaka huu. “Tunajivunia jinsi ambavyo watanzania wanatuunga mkono kwa miaka sasa. Tunaona vyema tuwapatie kile kinachostahili ili wao pia wajisikie kuwa sehemu ya familia ya Vodacom Tanzania. Ninawaahidi kuwa tutaendelea kuwapatia kile wanachohitaji ili wajisikie vizuri sasa hata baadae,” aliongeza Meza.





No comments:

Post a Comment