Tuesday, May 15, 2018

TUKIO LA CAREER DAY, MOSHI ,LAWAKUTANISHA WAHITIMU NA WAAJIRI


PICHANI : Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira (katikati) akiwa ameongozana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) Prof, Faustine Bee ( mwenye tai) alipowasili chuoni hapo kwa ajili ya tukio la Career Day ,tukio ambalo Mghwira alikuwa mgeni rasmi .

Na Dixon Busagaga,Moshi

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) ,Prof, Faustine Bee ameshauri kuanzishwa kwa ujasiliamali wa Kiushirika utakao saidia wahitimu wa vyuo vikuu nchini kujipatia kipato na kuongeza kasi ya ukuzaji wa Uchumi kabla ya kupata ajira ya kudumu.

Katika maadhimisho ya siku hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwl Nyerere uliopo chuoni hapo ,Prof Bee alitolea mfano, moja ya changamoto zilizopo kwa baadhi ya vyama vya ushirika kwa kukosa wataalamu wa kuweka vizuri hesabu ya vitabu vyao.

“Pamoja na juhudi hizi binafsi za kwenda kutengeneza ajira na kuanzisha ujasiliamali wa mtu mmoja mmoja ,ni vema sasa tuone namna ambavyo tutaanzisha ujasiliamali wa kiushirika kwa maana wahitimu wa chuo kikuu wanapo maliza waende kuanzisha vyama vya ushirka vya aina tofauti.”alisema Prof Bee.

“Kuna vyama vina shida ya uandishi wa hesabu wa vitabu vyao ,tupate ambao watakuwa wakifanya kazi hiyo na watakuwa wakijipatia pesa,lakini pia wapo wengine ambao wangeweza kuanzisha vyama vya ushirika vya aina tofauti ,vya fedha, vya mazao ,vya uvuvi, ili mradi viongeze kasi ya ukuzaji wa uchumi wetu na pia kutengeneza ajaira kwa atu wengine .aliongeza Prof ,Bee.

Maadhimisho ya siku hii yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwl Nyerere uliopo chuoni hapo yalitanguliwa na maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na kuuzwa na wanafunzo wa chuo hicho pamoja na uwasilishaji wa mada ambapo mgeni rasmi katika tukio hilo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akaikumbusha menejimenti ya chuo sehemu ya wajibu wa chuo.

“Katika kujenga na kuimarisha fani ya ushirika ,Chuo Kikuu hiki cha ushirika ndicho kingekuwa kioo chetu ,kila siku tunasema tukitaka kuzungumza na wana ushirika twende Chuo Kikuu cha Ushirika ,tupate taarifa sahihi kutoka chuoni ,tupate taarifa za uchambuzi mzuri ,za tafiti mbalimbali kuhusiana na mazao mbalimbai yanayounda ushirika”alisema Mghwira .

Katika tukio la “Career Day” linalofanyika chuo kikuu cha Ushirika Moshi kila mwaka huku likiwakutanisha wanafunzi wanaotarajia kuhitimu masomo yao ya elimu ya Juu pamoja na waajiri kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wahitimu wakizilinganisha na masomo waliyojifunza.

Tukio la Career Day huandaliwa na serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi kwa kushirikiana na ofisi ya Makamu mkuu wa chuo hicho ,utawala na fedha kwa lengo la kuwaonyesha waajiri shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi hao zikiambatana na masomo yao .

Baadhi ya Wanafunzi na wageni mbalimbali waliohudhuria tukio la Career Day lililofanyika katika ukumbi wa Mwl Nyerere ,Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza wakati wa tukio la Career Day alipoalikwa kuwa mgeni rasmi ,tukio hilo limefanyika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU)









Baadhi ya Wananfunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU).



Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) Prof,Faustine Bee akizungumza katika tukio hilo .



Baadhi a wanafunzi wa MOCU



Naibu Makamu Mkuu wa Chuo,Utawala na Fedha wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MOCU) Prof Freddy Kilima akizungumza wakati wa tukio la Career Day .



Baadhi ya Wageni walioalikwa kushiriki tukio la Career Day kutoka nchini Sweden .



Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MOCU) Nalemuta Ngoitiko akizungumza katika tukio hilo.



Naibu Makamu Mkuu wa Chuo,Taaluma Prof,Alfred Sife akitoa neno la shukrani wakati wa tukio la Career Day lililoandaliwa na serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU).











Mgeni rasmi katika tukio hilo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira alipata nafasi ya kutembelea mabanda ya maonesho yaliyoandaliwa na baadhi ya wanafunzi wanaosoma fani mbalimbali katika chuo kikuu cha Ushirika ,Moshi.



Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ,Pro Faustine Bee wakifurahia kazi ya Sanaa ya uchoraji iliyofanywa na mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa Shahada ya Sheria katika chuo hicho ,Omega Lyimo



Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ,Prof Faustine Bee ni kama aamini baada ya kuona picha yake iliyochorwa na Mwanafunzi Omega Lyimo.



Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tukio la Career Day,Onesmo Mbisse akikabidhi zawadi ya T shirt zenye nembo ya chuo hicho kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira .



Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tukio la Career Day,Onesmo Mbisse akikabidhi zawadi ya T shirt zenye nembo ya chuo hicho kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Prof Faustine Bee.





Mwisho.


No comments:

Post a Comment