Thursday, September 28, 2017

SERIKALI YAIPONGEZA COSTECH-OFAB KWA KUANDAA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA SAYANSI 2017


Mwandishi wa Habari wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu akipeana mkono na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa kwanza kwenye kuandika na kuelimisha umma kuhusu matumizi ya sayansi, Teknolojia na ubunifu hususani Bioteknolojia katika kuendeleza kilimo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Hassan Mshinda


Washindi wa tuzo hizi wakisubiri kutangazwa.


Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.


Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Jim Yonaz akitoa hutuba katika hafla hiyo.


Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyindondi akielezea tuzo hizo


Mkurugenzi Mkuu wa COTECH, Dk.Hassan Mshinda akizungumzia tuzo hizo


Waziri Ndalichako akihutubia katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk.Ayoub Rioba akizungumza kwenye hafla hiyo.




Mshindi wa tuzo hizo kutoka mkoani Kagera, Benson Eustace wa Clouds Media kikabidhiwa cheti chake.




Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Jim Yonaz akikabidhiwa cheti kutokana na mchango mkubwa wa vyombo hivyo katika kuandika habari za sayansi.




Mwakilishi wa TBC, akikabidhiwa cheti kutokana na mchango wa kuandika habari za sayansi.




Ofisa Mawasiliano wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha SUA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Kujiendeleza (ICE), Bujaga Inzengo Kadago akipokea cheti kutokana na mchango wa vyombo vya habari vya chuo hicho wa kuandika habari hizo.




Mwanahabari wa gazeti la Habari Leo, Lucy Ngowi akikabidhiwa cheti.




Mwanahabari Hellen Kwavava akikabidhiwa cheti.




Mwanahabari wa Gazeti la Nipashe mkoani Kagera, Restuta Damian akipokea cheti.




Mwanahabari wa gazeti la Guardian, Daniel Simbei akipokea cheti.




Mwanahabari Calvin Gwabara kutoka SUA akipokea cheti.




Mwanahabari wa gazeti la Daily News, Fatma Abdul akipokea cheti.




Mwanahabari Elias Msuya wa Gazeti la Mwananchi akikabidhiwa cheti.




Mwanahabari wa RFA kutoka Mwanza, Coleta Makulwa akipokea cheti






Mwanahabari wa gazeti la Habari Leo, Shadrack Sagati

akikabidhiwa cheti.

Mwanahabri Dino Mugunde wa Star TV Mwanza akipokea cheti.




Waziri Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na washindi.


Mshindi wa kwanza wa tuzo hizo, Gerald Kitabu akitoa shukurani zake.







Mwanahabari Calvin Gwabara kutoka SUA, akipongezwa na dada yake huku akionesha vyeti vyake.










Na Dotto Mwaibale






WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka waandishi wa habari nchini kutumia taaluma zao kuelimisha jamii kuhusu habari za sayansi na teknolojia ili kuleta maendeleo nchini.






Akizungumza wakati wa utoaji tuzo za umahiri katika uandishi wa habari za Sayansi zilizoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknlojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknojia (OFAB), Waziri Ndalichako alisema tuzo hizo iwe ni chachu za kuandika habari za sayansi kwa undani ili kuwajengea uelewa wananchi wa.kawaida.






Alisema ufundi wa waandishi katika.kuandika habari za sayansi utasaidia kutangaza ubunifu na kuongeza tija thamani katika teknolojia mbalimbali.






"Wananchi wanahitaji teknolojia za kisasa katika kurahisisha utendaji kazi hivyo uandishi wenu utasaidia kuinua sekta ya kilimo na mifugo ambayo ndio kundi.muhimu katika jamii hasa katika kuelekea uchumi wa viwanda,"alisema Ndalichako.






Aliwataka Costech na taasisi nyingine kuendelea kushirikiana na wanahabari kuelimisha jamii katika masuala ya sayansi.






Ndalichako alipongeza COSTECH na OFAB kwa kuandaa tuzo hizo kwani zitaongeza mori kwa wanahabari wa kuandika habari za sayansi.


Akielezea ushiriki wa.waandishi katika shindano hilo lililoanza Januari hadi Agosti mwaka hii, Mkurugenzi Mkuu wa COTECH, Dk.Hassan Mshinda alisema, shindano hilo hapa nchini sasa ni mara ya tisa kufanyika na kwa upande wa Afrika ni la kumi.






Alisema katika shindano hilo jumla ya makala 200,vipindi vya radio 20 na televisheni 15 vilishindaniwa.






Mshindi alisema watalaam waliobobea ambao walifanyakazi ya.kutafuta washindi ambao walipata dola 250, 750, 1,000 na 1,500.






Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Jim Yonaz aliwataka waandishi kuwa daraja kati ya wana sayansi na jamii.






Alisema wana sayansi wana lugha ngumu hivyo kupitia waandishi na aina ya uandishi wao wamesaidia jamii kuelewa habari mbalimbali za sayansi.






"Katika kuchangia uchumi wa viwanda waandishi wanakazi kubwa kuhakikisha wanatoa elimu ya sayansi na kilimo ili kuelimisha jamii,"alisema Yonaz.






Yonaz pia aliiomba Serikali kuhakikisha inawawezesha waandishi kwa kuwajengea uwezo wa ufahamu ili waweze kuelewa zaidi sababu zinazowafanya kuandika habari mbalimbali.






Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk.Ayoub Rioba alisema, wana sayansi wana jukumu la kuboresha maisha ya jamii kwa kuhakikisha wanatumia zana zilizoboreshwa kiteknolojia.






Alisema kwa sababu ya lugha itumikayo na wana sayansi upo umuhimu wa wanahabari kuandika.habari nyingi za sayansi.






Rioba pia aliitaka taasisi ya Costech pamoja na taasisi nyingine kuendelea kufanya kazi za kuelimisha jamii kwa kushirikiana na wana habari ili kujenga jamii yenye uelewa wa masuala ya sayansi.






Miongoni mwa waliopata tuzo za umahiri wa habari za Sayansi ni pamoja na mshindi wa jumla Gerald Kitabu (Guardian), Shedrack Sagati(Habari Leo), Elias Msuya (Mwananchi), Calvin Gwabara, Fatma Abdul (Daily News) na Dino Mugunde.






Wengine ni Lucy Ngowi, Hellen Kwavava, Coleta Makulwa, Daniel Simbei, Benson Eustace na Restuta Damian.






(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

No comments:

Post a Comment