Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na mikakati waliochukua kukabiliana na kuondoa tatizo la maji machafu yanayotoka jijini Tanga ili kuhakikisha maji yanarudi kwenye hali yake ya kawaida lakini kulia ni Meneja wa Ufundi wa Mamlaka hiyo,Farles Aram
Kushoto mwenye tisheti ya njano ni Mwandishi wa Gazeti la Majira Mkoani Tanga,Mashaka Mhando akiuliza swali katikati ni Joachim Kapembe kutoka Shirika la Utangazaji la TBC na kulia ni Mwandishi wa ITV na Radio One Mkoani Tanga,Wiliam Mngazija.
MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)inapoteza kiasi cha shilingi milioni 13 kila siku kutokana na kuongezeka kwa za shughuli za kibinaadamu zinazofanywa katika vyanzo vya maji vilivyopo katika Mto zigi na Muzii Wilayani Muheza.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kwenye vyanzo vya maji, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa alikiri kuwepo kwa uharibifu mkubwa katika vyanzo hivyo unaosababishwa na wananchi katika maeneo hayo.
Mhandisi Mgeyekwa alisema shughuli za uchimbaji wa dhahabu,kilimo na maogesho ya mifugo katika vyanzo hivyo vimekuwa vikichangia kwa kiasi kikubwa kuongeza matope kwenye bwawa la Mabayani linalosambaza maji Mjini hasa kipindi hiki cha mvua za masika.
Aidha alisema kuwa awali mamalaka hiyo ilikuwa inazalisha maji kiwango cha ujazo km 29,000 na kupungua hadi kufikia ujazo wa km 20,000 kwa sasa jambo lililopelekea kuanza kutoa huduma hiyo kwa mgao ndani ya Jiji la Tanga.
Alisema wao kama mamlaka baada ya kugundua kuwepo kwa tatizo hilo walianza kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuvitembelea vyanzo vyote vya maji ili kubaini uhalisi uliopo na namna ya kuanza kulishughulikia jambo hilo kwa haraka zaidi ili lisiweze kuleta madhara kwa wananchi.
“Ki ukweli tatizo hili la katizo la maji na maji kutoka machafu haliwaathiri wananchi peke yake hata sisi kwenye maeneo yetu tunayokaa limekuwa likijitokeza hivyo tunaangalia namna ya kupambana nalo usiku na mchana kwa lengo la kutatua shida hiyo”Alisema.
Mkurugenzi huyo alisema tayari mamlaka hiyo imekwisha kuanza kuchukua jitihada za haraka ikiwemo kutumia maji ya kisima cha mwakileo ambacho kina uwezo wa kutoa maji kwa ujazo wa km 30,000 hadi 35,000 ambayo yanaweza kukidhi mahitaji ya zaidi wananchi 47,000 kwa wakati mmoja sambamba na kuzibua mabomba ambayo yamekuwa na tope iliyosababishwa na mvua zinazoendelea sasa.
Hata hivyo aliwataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji kwani kufanya hivyo kunasababisha madhara makubwa kwa watumiaji wake ikiwemo kupungua kina cha maji na maji kutoka machafu jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.
Akizungumza wakati wa ziara ya waandishi wa habari walio tembelea vyanzo vya maji vya Mto Muzii,Zigi,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watumiaji wa Maji Zigi Juu,Philipo Mdoe alisema hali ya uchafuzi wa maji na kupungua kina kumechangiwa kwa asilimia kubwa na shughuli za kibinadamu zinazofanywa karibu na vyanzo hivyo jambo ambalo jitihada za haraka zisipochukuliwa kunaweza kukaleta athari zaidi kwa wananchi.
“Tunaiomba mamlaka kwa kushirikiana na serikali kupitia vyombo vya dola vifanye operesheni za kushtukiza mara kwa mara kwani hii itasaidia kupunguza ama kuondokana na uchafuzi wa mazingira unaofanywa na watu kwenye nyanzo hivyo “Alisema.
Awali akizungumza katika mkutano huo,Mratibu wa Mazingira Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Nyambuka Ramadhani alisema suala la utunzaji wa vyanzo vya maji ni wajibu kwa jamii kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri wa kuona namna ya kuvilinda ili visiweza kuharibiwa.
“Lazima jamii itambua umuhimu wa kuvitunza na kuvilinda vyanzo vya maji kwani bila hivyo wanaweza kukumbwa na athari za kukosekana kwa maji au kupatikana kwa maji yasiyokuwa safi na salama hivyo tushirikiana kupambana na waharibifu wa mazingira “Alisema.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Citizeni Mkoani Tanga, George Sembony kulia akiuliza swali kwenye mkutano huo kushoto ni Mwandishi Zawadi Kika wa Clouds TV
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo kulia ni Mwandishi wa Gazeti la Citizeni George Sembony
Mratibu wa shughuli za Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah akizungumza jambo kwenye mkutano huo
Baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo wakifuatilia mkutano huo na waandishi wa habari leo
Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakichukua habari
Joachim Kapembe kutoka Shirika la Utangazaji la TBCkushoto akiwa sambamba na mtumishi wa mamlaka ya Maji Tanga Uwasa wakiingia kwenye kituo cha kusafishia Maji cha Moye
Waandishi wa habari wakitazama namna maji yaliyohifadhiwa kwenye kituo cha kusafishia maji cha Mowe kabla ya kufika kwa walaji wa kwanza ni Sophia Wakati wa Gazeti la Uhuru wa pili ni Mbaruku Yusuph wa gazeti la Tanzania Daima
Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania,Sussan Uhinga naye akiangalia namna maji yanavyosafishwa kabla ya kuwafikia walaji
Waandishi wa Habari wakiongozwa na Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania wakitembelea eneo la kusafishia maji kabla ya kufika kwa watumiaji la
Eneo la Mowe ambalo maji huchujwa kabla ya kuwafikia walaji
Mwandishi wa gazeti la Mtanzania,Sussan Uhinga na Frank wa TK wakiwa kwenye eneo hilo kujionea
Mratibu wa shughuli za Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah akizungumza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu dawa ambazo zinatumika kuwekwa kwenye maji
Mratibu wa shughuli za Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah akiwaonyesha mitambo iliyopo kwenye kituo hicho wakati walipoitembelea kujionea
Waandishi wakitoka kulia ni Mashaka Mhando wa gazeti la Majira Mkoani Tanga kushoto ni William Mngazija wa ITV na Radio One Mkoani Tanga
William Mngazija wa ITV na Radio One Mkoani Tanga akiwa ongoza waandishi wengine kuingia kwenye vyanzo vya maji kuona namna hali ilivyo
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Citizeni Mkoani Tanga, George Sembony akiwa kwenye vyanzo hivyo vya maji
Muonekano wa Maji kwenye chanzo cha Maji cha Mto Zigi
No comments:
Post a Comment