Thursday, February 02, 2017

TIMU YA WANAHABARI IRINGA YAPIGWA JEKI NA MBUNGE RITTA KABATI

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) akimkabidhi mwenyekiti wa waandishi wa habari mkoani Iringa moja ya jezi alizotoa kwa waandishi wa habari kwa ajili ya mechi mbalimbali za timu hiyo

na fredy mgunda,Iringa

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) ameipiga jeki timu ya wandishi wa habari mkoa wa Iringa kwa kuwapatia jezi seti moja ,mpira na pesa taslim kiasi cha Tsh 50O,000 ili viwasaidie katika malengo yao ya kukipiga ligi daraja la kwanza .

Akikabidhi msaada huo kwa mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard juzi mbunge huyo alisema kuwa yeye kama mlezi wa timu hiyo ameamu kujingiza kwa miguu yote kuisaidi timu hiyo ambayo inaonekana kufanya vema kwenye mchezo wa soka mkoani hapo .

Kabati alisema kuwa licha ya kuwa mpira ni ajira pia unamsaidia mtu kuwa na afya njema itakayomsaidia kujiepusha na magonjwa yanayoepukika ikiwemo presha .


“Niwatie moyo hichi mulichokianzisha ni kizuri na timu yenu ina fanya vizuri na juzi tu mumenyakua kombe la Spanest kwa kuwanyuka kitisi huu ni ushahidi tosha mukiendelea hivi hivi mutakuja kuingia ligi daraja la kwanza na baadaye ligi kuu .

Kabati aliwataka wadau wengine mkoa Iringa na nje ya Iringa kuendelea kujitolea kuisaidia timu hiyo ya wanahabari ili iendele kufanya vema ndani na nje ya mkoa wa iringa

Akipokea vifaa hivyo mwenyekiti wa wanahabari mkoa wa Iringa Frank Leonard alimshukuru mbunge huyo kwa vifaa na fedha alizotoa huku akimuahidi mbunge huyo kuwa timu hiyo itakipiga na timu mbalimbali ikiwemo timu ya bunge la jamuhuri wa muungano wa Tanzania

Frank alisema kuwa timu hiyo imekuwa ikifanya vema kutokana na kuwa na wandishi wazuri vijana waliona ari ya kusakata kambumbi hivyo ni vema timu ya bunge kujipanga kisawasa kwani hawata toka salama pindi watakapokipiga nao mjini dodoma

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) ameipiga jeki timu ya wandishi wa habari mkoa wa Iringa kwa kuwapatia jezi seti moja ,mpira na pesa taslim kiasi cha Tsh 50O,000 ili viwasaidie katika malengo yao ya kukipiga ligi daraja la kwanza .







No comments:

Post a Comment