Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo(wa pili kutoka kulia) na Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi ,George Mkanza wakikabidhi hundi ya kodi ya huduma ya zaidi ya Sh Mil 740 kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Fadhili Nkurlu(wa pili toka kushoto) tukio lililofanyika juzi mjini Kahama ,Wa kwanza kushoto ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kahama Bi Marry Manyambo.
Mkuu wa Wilaya Kahama,Fadhili Nkurlu na akimkabidhi hundi iliyotolewa na Mgodi wa Buzwagi kama Kodi ya Huduma yenye thamani ya zaidi ya Sh Mil 740 , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa hospitali kubwa ya wilaya ya Kahama, mradi ambao ujenzi wake utategemea fedha zinazotokana na kodi za ushuru wa huduma unaolipwa na Mgodi huo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.
HALMASHAURI
ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga imepokea kiasi cha Sh Mil 700,040,000
kutoka kwa kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi
ikiwa ni sehemu ya kodi ya huduma (service levy) ya kipindi cha mwezi
Julai na Desemba 2016.
Kiasi hiki ni zaidi ya kilichotolewa
kipindi cha Julai na Desemba mwaka 2015 ambapo mgodi huo uliikabidhi
halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye thamani ya kiasi cha sh Mil
500,088,000 kama kodi ya huduma ikiwa ni utekelezaji wa sheria kwa
kulipa kodi zilizopo kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza wakati wa
hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi ,Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi
Mhandisi Asa Mwaipopo alisema Buzwagi inamatumaini makubwa kuwa katika
siku za karibuni halmashauri itaanza kutekeleza mradi huo na hivyo kutoa
matumaini kwa wananchi wa Kahama kupata huduma nzuri za afya ndani ya
wilaya.
“Mpaka sasa kama Kampuni tumekwisha kabidhi kwenu
takribani kiasi cha bilioni 1.4 hii ikiwa na maana ya kodi yote ya
ushuru wa huduma katika kipindi cha mwaka 2016, wananchi wangetamani
kuona mradi huu unaanza maana kiasi hicho kilichopo kama kitatumika
kinaweza kutekeleza sehemu kubwa ya mradi huu kwa kuanzia wakati
tukisubiri awamu zingine” alisema Mwaipopo.
Katika hafla hiyo ya
makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya makazi ya viongozi katika
wilaya hiyo,Mwaipopo alisema licha ya Kampuni yake kulipa kodi
mbalimbali bado imekuwa ikijishughulisha katika kuhakikisha inakuwa mdau
muhimu wa maendeleo kwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo katika
maeneo yanayozunguka Mgodi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya
Kahama ,Fadhili Nkurlu aliyepokea hundi hiyo kutoka kwa uongozi wa
Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama
ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa
wakizifanya katika kuhakikisha wanalipa kodi mbalimbali pamoja na
jushirikiana na Jamii katika kutekeleza miradi mbalimbali.
Alisema
Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi umeekua mstari wa mbele katika kulipa kodi
mbalimbali ambako mpaka kufikia sasa zimefikia zaidi ya shilingi bilioni
197 ambazo zimetolewa katika vipindi tofauti.
Akizungumzia
matumizi ya pesa hizo katika kutekeleza mradi wa ujenzi wa hospitali ya
wilaya ya Kahama Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson
Msumba alisema halmashauri iko katika hatua za mwisho za utekelezwaji wa
ujenzi huo.
Miloni 700,040,000 zilizotolewa zinafanya juma ya
pesa zote zilizotolewa katika vipindi vya miaka miwili kufikia Bil 1.2
fedha ambazo zitasaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ukiwemo
wa Afya.
Baadhi ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama wakifuatilia hafla ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya mji wa Kahama.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akiwahutubia waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya Kahama pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Mji wa Kahama
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (aliyesimama) akihutubia wageni waalikwa wakati wa hafla ya kupokea hundi ya ushuru wa huduma kutoka Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. Kutokea kushoto waliokaa ni Katibu tawala wa wilaya Kahama Timothy Ndanya na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo.
Mkuu wa wilaya Kahama na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi wakiteta jambo.
No comments:
Post a Comment