MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi huku wananchi wakiwa kwa pembeni
na fredy mgunda,iringa
Gari la kubebea wagonjwa [Ambulance] lenye thamani ya mill.80 lakabidhiwa katika kwa mkurugenzi na mkuu wa wilaya wa Mufindi na MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa ametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.
Mgimwa alikabidhi gari hilo ikiwa ni moja ya ahadi yake aliyoitoa wakati akiomba kura kwa wananchi wa jimbo la mufindi kaskazini katika kampeni ya uchaguzi mkuu 2015,ambapo alisema kutokana na changamoto ya uhaba wa gari ya kubebea wagonjwa katika zahanati na vituo vya afya katika jimbo hilo, endapo atapewa ya kuwa mbunge atahakikisaha gari ya wagonjwa linapatikanaili wagonjwa waweze kufika hospital kwa wakati.
Akizungumza na wananchi wakati wa kukabidhi gari hilo,mbunge Mgimwa alisema muda wa kupiga siasa umeshapita na kazi iliyopo hivi sasa ni kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwatatulia changamoto zinazowakabili.
Alisema pamoja na kuongeza gari ya wagonjwa atahakikisha anaboresha vituo vya Afya vilivyopo katika jimbo lake ili kupunguza wimbi kubwa la msongamano wa wagonjwa wanaokuja kutibiwa katika Hospitalini ya wilaya.
‘’’Nipo kwenye mchakato wa kuboresha vituo vyote vya Afya ndani ya jimbo langu,na nitahakikisha huduma muhimu zinapatikanaikiwa pamoja na dawa za kutosha na vifaa mbalimbali vinavyohitajika ili wananchi wangu waweze kuhudumiwa bila usumbufu katika vituo hivyo,hii itasaidia kupunguza msongamano katika hospitali ya wilaya’’’’’alisema Mgimwa
Aidha katika mkutano huo mbunge alisisitiza swala la uaminifu kwa watumishi waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi wahakikishe wanajikinga na vitendo vinavyoashiria rushwa ,vinavyoweza kuwaharibia sifa ya utendaji kazi zao na kushindwa kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao.
‘’’Sisi wabunge,madiwani na mtumishi yeyote aliyepewa dhamana na wananchi anatakiwa ajiepushe na swala zima la rushwa ili aweze kutenda haki kwa kuwatatulia changamoto wananchi wake waliomchagua. Tunatakiwa tuwatumie wananchi kuwaletea maendeleo ipasavyo na si vinginevyo’’’alisema
Jamhuri William ni mkuu wa wilaya ya Mufindi,akipokea msaada wa gari hilo kutoka kwa mbunge Mgimwa alisema gari hilo litaweza kusaidia kuokoa vifo vya wanamufindi hasa mama na mtoto ambapo hapo awali kuliwa na gari moja tu.
Williamu alisema kutokana na uwingi wa wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika hospitali ya wilaya kwa mwezi ni zaidi ya 500 aliosimia kubwa ni akina mama wajawazito na wengi wao wanafikishwa wakiwa katika hali mbaya kutokana na gari la wagonjwa kuwa moja na kushindwa kumudu.
“Tunamshukuru mbunge kwa kuliona hili na na kuokoa maisha ya watu hasa mama na mtoto ingawa bado hitaji lipo kutokana na uwingi wa wagonjwa endapo tutapata gari la tatu itasaidia sana”alisema
Williamu ameongeza kwa sasa gari hilo litahudumiwa na wilaya kuanzia kuwalipa wafanyakazi wa gari hilo,kulifanyia marekebisho ya gari hilo endapo litatokea kuharibika kwa aina yoyote ile.
Wananchi nao walitoa malalamiko yao kwa mbunge Mgimwa,ambapo Markusi Chusi alimuomba mbunge aweze kusiomamia swala la utapikananji wa vibali vya kuvuna miti,kwa kumtaka ahakikishe wazawa wa eneo husika wanapewa kipaumbele ili waweze kunufaika mali alisi hiyo ilipo kwako.
‘’’’Tumelia kwa muda mrefu,sisi tunanyanyasika kwa kuwapendelea wageni na kutuacha sisi wenyeji tuliopo hapa.Nimeomba mara tano hivi sasa na ukizingatia mimi ni mjane lakini naachwa na pesa yangu inaliwa wageni wanapewa hali inayotukatisha tama wananchi tuliouzunguka msitu huu.’’’’alisema
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akifurahia jambo na viongozi wa wilaya ya mufindi MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa na viongozi wa wilaya ya mufindi wakiangalia muonekano wa wa gari hilo la kubebea wagonjwa na hii ndio sehemu ya ndani ya gari la kubebea wagonjwa alilokabizi mbunge wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi.

No comments:
Post a Comment