Sunday, August 28, 2016

DC MTATURU AWATAKA WANANCHI WALIOVAMIA ENEO LA HIFADHI KUHAMA NDANI YA MWEZI MMOJA

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugere Beatus Kapatya akitoa taarifa juu ya kusimama kwa ujenzi wa Zahanati hiyo.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa Makini Mkuu wa Wilaya ya ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaugeri wakati akitoa maelezo wakati wa kikao cha serikali ya kijiji

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali wakati wa ziara yake Wilayani humo
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugere Beatus Kapatya akitoa ufafanuzi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
Umakini wa wananchi ukiwa umetawala wakati wa Mkutano wa Kijiji, Wilayani ikungi

Na Mathias Canal, Singida

Serikali ilitangaza eneo la Hifadhi ya msitu wa wananchi waliomo ndani mwaka 2003 ambao kutangazwa huko kuliashiria wananchi kuhama katika maeneo hayo ili kutoa fursa kwa serikali kusimamia kwa karibu eneo hilo lakini wananchi hao mpaka sasa hawajahama kwa kukaidi agizo hilo.

Jambo hili limemsukuma Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kufanya ziara na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo kwa lengo la kuwaelemisha juu ya uvunjaji sheria za nchi kwa kuendelea kusalia katika maeneo ambao wametakiwa kuhama jambo ambalo kama watashindwa kulitekeleza serikali itawatoa kwa nguvu kwani kwa kiasi kikubwa wanaharibu mazingira.

Akizungumza na Wananchi hao katika Kijiji cha Kaugeri Kata ya Mwaru Wilayani hapa Dc Mtaturu ametoa mwezi mmoja kwa wananchi hao kuhama haraka iwezekanavyo ili kupisha eneo hilo la Hifadhi ya msitu kufanya Kazi iliyokusudiwa kwa zaidi ya miaka kumi sasa.

Mtaturu amesema kuwa Kwa mujibu wa sheria Kijiji kinapaswa kutoa Ardhi hekari zisizozidi hamsini kwa mwekezaji lakini uongozi wa Kijiji hicho umegawa kwa mwekezaji hekta 150 hadi 200 kinyume kabisa na taratibu za kiutendaji ukiwa ni pamoja na kuingia mikataba ya kinyonyaji.

Pamoja na hayo pia viongozi hao wametoa Ardhi hiyo bila kushirikisha wananchi jambo ambalo limeibua hisia Kali kwa wananchi ambao wanatambua uporwaji huo wa maeneo yao.

Kufuatia kadhia hiyo ya viongozi hao kugawaji Ardhi kinyume na taratibu Dc Mtaturu amewaweka lumande Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaugeri Mange Nkuba, Aliyekuwa Kaimu Afisa Mtendaji Laurent Bomba, na mjumbe wa serikali ya Kijiji Paul Kilo huku Amani Clement ambaye alitoweka kabla Ya mkutano kumalizika anaendelea kutafutwa mpaka apatikane.

Katika hatua nyingine Dc Mtaturu ameagiza mkandarasi Samwel John kukamatwa na kuhojiwa kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji tangu Mwaka 2013 ambapo tayari alishapewa kitita cha shilingi milioni 19 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.

Hata hivyo pamoja na mkandarasi kukabidhiwa fedha hizo alianza ujenzi lakini jengo hilo halijafika hata kwenye Renta huku likiwa limejengwa chini kiwango.

Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi amemuagiza mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya hiyo kupitia idara ya ujenzi kutoa taarifa kwanini hawakushiriki kutoa huduma za kiutaalamu katika kusimamia jengo hilo la umma kabla na wakati ujenzi unaanza.


No comments:

Post a Comment