Na. Aron Msigwa - Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha Makatibu Tawala wapya wa mikoa 10 aliowateua Aprili 25 mwaka huu katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John William Kijazi.
Makatibu Tawala walioapishwa leo ni Bw. Jumanne Abdallah Sagini ambaye anakwenda kuwa Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Selestine Muhochi Gesimba Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Geita na Dkt. Thea Medard Ntara Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Tabora.
Wengine ni Mhandisi Zena Said ambaye anakwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Albert Gabriel Msovela Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Shinyanga, Dkt. Angelina Mageni Lutambi aliyeapishwa kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Singida, na Dkt. Angelina Mageni Lutambi ambaye anakwenda kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Singida.
Pia amewaapisha Bw. Richard Kwitega kuwa Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Arusha, Bw. Armatius C. Msole kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Mhandisi Aisha Amour ameapishwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro na Bw. Zubeir Mhina Samataba aliyeapishwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani.
Mara baada kuapishwa Makatibu Tawala hao wamejaza fomu za Maadili kwa viongozi wa umma zinazowataka wazingatie Sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Utumishi wa Umma.
Akizungumza na Makatibu Tawala hao mara baada ya kukamilisha zoezi la ujazaji wa fomu hizo Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John William Kijazi amewataka wazingatie maadili na mipaka yao ya kazi na kuepuka kuwabagua watumishi wanaowaongoza.
Balozi Kijazi amewataka waishi kwa kufuata miiko na maadili kwa viongozi wa umma yaliyoanishwa kwenye fomu walizojaza ili kuepusha mgongano wa kazi na maslahi mahali pa kazi.
Amewaagiza Makatibu Tawala hao kuwasimamia watumishi walio chini yao ili maadili waliyokubali kuyazingatia yafuatwe na watumishi walio chini yao.
“Napenda kuwajulisha kuwa tuko kwenye awamu nyingine, na mnajua kuwa awamu hii ikisema jambo maana yake litekelezwe, msije mkaliacha mezani na kuendelea na mambo mengine” Amesisitiza Balozi Kijazi.
Amewataka Makatibu Tawala hao kushirikiana kikamilifu na watumishi wanaowaongoza ili waweze kutatua kero mbalimbali za wananchi kwa kuyashughulikia kwanza matatizo watakayoyakuta katika vituo vyao kabla ya kuanzisha mambo mapya.
Kwa Upande wao Makatibu Tawala walioapishwa wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wamejipanga kikamilifu kutekeleza kwa vitendo Kauli mbiu ya “Hapa Kazi Tu” kwa kuwatumikia wananchi katika maeneo waliyopangiwa.
Bw. Zubeir Mhina Samataba aliyeapishwa kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Pwani amesema kuwa katika uongozi wake atahakikisha kuwa anashirikiana na watumishi wenzake kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa mkoa wa Pwani.
Amesema kuwa ataweka mkazo katika kuwahamasisha wananchi kufanya kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo ya kiuchumi, kukuza sekta ya kilimo cha mazao ya Chakula, Biashara na Elimu mkoani Pwani.
Aidha,amesisitiza kuwa anakwenda kulisimamia kikamilifu suala la uhakiki wa Watumishi hewa katika mkoa wake pamoja na kushughulikia migogoro ya ardhi iliyo katika mkoa wa Pwani.
Naye Dkt. Angelina Mageni Lutambi ambaye aliyeapishwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Singida akizungumza mara baada ya kuapishwa amesema kuwa jukumu lililo mbele yake ni kuhimiza uchapakazi miogoni mwa watumishi wa mkoa wa Singida.
“Nimelipokea jukumu hili nililokabidhiwa na Mhe. Rais kwa Moyo wa dhati, nitahakikisha kuwa ninawatumikia wananchi na kuwahimiza viongozi wenzangu kutimiza wajibu wao ipasavyo” Amesisitiza Dkt. Angelina Lutambi.

No comments:
Post a Comment