Wednesday, April 13, 2016

KOBE BRYANT KUSTAAFU, ATAENDELEA KUHESHIMIKA KATIKA MICHEZO

Kobe Bryant, aliyeisaidia timu ya Lakers kushinda mara tano kwa kunyakua makombe ya NBA katika miaka 20 ya kucheza mpira wa kikapu Los Angeles nchini Marekani, alitangaza rasmi siku ya jumapili katika mtandao wa Tribune kwamba atastaafu baada ya msimu huu.

Kwa mara ya kwanza katika habari yake mwenyewe yenye kichwa cha habari “Dear Basketball ( Mpendwa Mpira wa Kikapu”, Kobe mwenye umri wa miaka 37 alisema “msimu huu ndio pekee niliobakiza”

Katika mfumo wa mashairi, aliandika “kumpa mtoto wa miaka 6 ndoto yake ya Laker/ na nitaendelea kukupenda kwa hilo.”

“Lakini siwezi kuendela kukumiliki tena” Bryant aliandelea kuwa msimu huu ndio pekee niliobakiza. Moyo wangu unaaweza kuhimili kishindo. Mawazo yangu yanaweza kuvumilia msukosuko, lakini mwili wangu unajua kuwa ni muda wa kusema kwaheri. Na ni sawa tu, niko tayari kuachia.









No comments:

Post a Comment