Friday, April 15, 2016

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 248.477

Na Mwandishi Wetu

BARAZA la Madiwani la Halmashau ya Manispaa ya Kinondoni, limeidhinisha bajeti ya zaidi ya sh. bilioni 248.477 kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 ambapo zaidi ya sh. bilioni 64.285 ni makusanyo ya mapato ya vyanzo vya ndani vya manispaa.

Taarifa iliyosomwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Boniface Jacob Dar es Salaam jana, ilisema kuwa katika bajeti hiyo zaidi y ash. bilioni 182.771 ni mapato kutokana na ruzuku kutoka serikali kuu, zaidi ya sh. bilioni 1.420 ni mapato kutokana na michango ya nguvu za wananchi n ash.biliioni 12.281 ni mapato kutokana na fedha za mfuko wa barabara.

Meya alisema kuwa bajeti ya mapato ya ndani imelenga kutatua changamoto zilizopo na imeongezeka kutoka bilioni 56.550 hadi sh. bilioni 64. 285 ambalo ni ongezeko la sh. bilioni 7.7134 kutokana na vyanzo vya kodi ya majengo, mabango, huduma ya jiji, leseni za biashara na hoteli.
Alisema bajeti imeandaliwa kwa kuzingatia sera na miongozi ya kitaifa, sheria ya bajeti namba 11ya mwaka 2015, Duira ya Taifa ya maendeleo ya 2025, malengo ya millennia, mkataba wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA), Ilani ya CCM ya mwaka 2016/2021.
“Ambapo mpango wa tekeleza kwa matokeo makubwa sasa (BRN), sera ya Taifa ya Ukimwi, Mipango shirikishi jamii ya fursa na vikwazo kwa maendeleo (O$OD) ya Kata na Mitaa na sheria ya taa sura fedha ya serikali za mitaa 290 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010,”alisema.
Alisema katika sekta ya elimu Manispaa ya Kinondoni imetenga zaidi y ash. Bilioni 10 ili kwa kushirikiana na serikali kuu zitekeleze kwa vitendo sera ya elimu bure kwa kushughulikia changamoto mbalimbali kama upungufu wa Madarasa.

“Pia kushughulikia changamoto ya madawati, matundu vya vyoo, vifaa vya maabara na ukarabati wa miundombinu mibovu sambamba na uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mfuko wa wanawake na vijana,”.


No comments:

Post a Comment