WASHINGTON, Aprili 11, 2016
—
Shughuli za kiuchumi katika bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara
zilidorora katika mwaka 2015, wakati ukuaji wa Pato Ghafi la Taifa ukiwa
wa wastani wa asilimia 3.0, ikishuka
kutoka asilimia 4.5 mwaka 2014. Hii ina maana kwamba kasi ya ukuaji
uchumi imepungua hadi kufikia viwango vya chini tulivyovishuhudia kwa
mara ya mwisho mwaka
2009.
Takwimu hizi zimewasilishwa kwa muhtasari katika ripoti ya
Africa’s Pulse (Mapigo ya Damu ya Afrika),
huu ni uchambuzi wa kila nusu mwaka unaofanywa na Benki ya Dunia wa
mienendo ya kiuchumi na takwimu za hivi karibuni kwa bara hili. Makisio
ya ukuaji kwa mwaka 2016 yanabaki kuwa chini katika asilimia
3.3, kiwango ambacho kiko chini sana ukilinganisha na ukuaji imara wa
Pato Ghafi la Taifa kwa asilimia 6.8 ambao bara liliuendeleza kwa
kipindi cha 2003-2008. Kwa ujumla, ukuaji wa uchumi unatarajiwa
kuongezeka katika mwaka 2017-2018 kufikia asilimia 4.5.
Kushuka
kwa bei za bidhaa – hususani mafuta, ambayo yalishuka kwa asilimia 67
kutoka Juni 2014 hadi Desemba 2015 – na mdororo wa uchumi duniani, hasa
katika chumi za masoko yanayoibukia,
ndio sababu za bara kufanya vibaya kiuchumi. Mara nyingi, athari hasi
za bei za chini za bidhaa zimeongezewa nguvu na mazingira mabovu ya
ndani ya nchi kama vile mgawo wa umeme, sera zisizo na uhakika, ukame,
na vitisho vya usalama, ambavyo vyote vimekwaza
ukuaji uchumi. Kuna baadhi ya maeneo ambako uchumi umeendelea kukua kwa
nguvu kama vile nchi ya Ivory Coast, ambayo inajivunia mazingira mazuri
ya sera na kuongezeka kwa uwekezaji, pia na nchi zinazoagiza mafuta
kama vile Kenya, Rwanda, na Tanzania.
Mazingira
ya nje yanayolikabili bara yanatarajiwa kuendelea kuwa magumu. Katika
nchi nyingi, ulinzi wa kisera ni dhaifu, hivyo kupunguza mwitikio wa
sera wa nchi hizi. Ucheleweshaji
wa kutekeleza marekebisho ya kuanguka kwa mapato kutokana na mauzo ya
bidhaa nje ya nchi, na hali ya ukame inayozidi kuwa mbaya ni vitu
vinavyohatarisha matarajio ya ukuaji wa uchumi kwa bara la Afrika.
”Wakati
nchi zinajirekebisha kukabiliana na mazingira ya dunia yenye changamoto
nyingi, juhudi madhubuti zitahitajika kuongeza uhamasishaji wa
rasilimali za ndani. Wakati
mwenendo wa kushuka kwa bei za bidhaa ukiendelea, hususani mafuta na
gesi, huu ni muda muafaka kwa kuzidisha kasi ya mageuzi yote ambayo
yatazibua uwezo wa kukua kwa uchumi wa Afrika na kuwapatia watu wa
Afrika umeme nafuu,”
anasema
Makhtar Diop, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika.
Nchi
nyingi zinatarajiwa kuwa na ukuaji wa uchumi wa wastani. Miongoni mwa
masoko mapya, ukuaji uchumi unatarajiwa kuongezeka nchini Ghana,
unaosukumwa na kuboreshwa kwa hisia
chanya za wawekezaji, kuzinduliwa kwa visima vipya vya mafuta, na
kupungua kwa matatizo ya umeme. Nchini Kenya, ukuaji uchumi unatarajiwa
kuendelea kuwa imara, ukichangiwa na matumizi katika sekta binafsi na
uwekezaji wa umma kwenye miundombinu.
Ongezeko
la shughuli linalokisiwa katika mwaka 2017-2018 linaakisi maboresho ya
taratibu katika chumi kubwa zaidi katika bara – Angola, Nigeria, na
Afrika Kusini – wakati bei
za bidhaa zikitengemaa na maboresho ya kukuza uchumi yakitekelezwa.
Majiji ya Afrika kama Injini za Kukuza Uchumi
Wakati
Afrika inapita katika kipindi cha ukuaji wa kasi wa miji yake, kuna
dirisha la fursa la kutumia uwezo wa majiji haya kama injini za ukuaji.
Kushuka kwa haraka kwa bei
za bidhaa na mafuta kumekuwa na athari hasi kwa nchi zinazozalisha
bidhaa hizo na hivyo kuashiria haja ya haraka ya kujenga uchumi anuwai
katika bara la Afrika. Kukua kwa miji inayosimamiwa vyema kunatoa fursa
kubwa ya kuwa kichochezi cha uchumi anuwai.
Ukuaji
wa majiji, kama utasimamiwa vyema, unaweza kusukuma ukuaji wa uchumi na
tija. Lakini majiji ya Afrika kwa sasa hayajengi chumi za mkusanyiko au
kuvuna faida za tija za
mijini. Badala yake yanasumbuliwa na gharama za juu za makazi na
usafiri, aidha na gharama za juu za chakula ambazo zinatumia sehemu
kubwa ya bajeti za kaya za mijini.
Makazi
na usafiri ni yenye gharama kubwa hususani katika miji ya Afrika. Bei
za makazi ni takribani asilimia 55 juu zaidi katika maeneo ya mijini ya
nchi za Kiafrika ukilinganisha
na viwango vyao vya kipato. Usafiri mijini, ambao unajumuisha bei ya
magari na huduma ya usafiri, ni takribani asilimia 42 ghali zaidi katika
miji ya Afrika kuliko ilivyo katika nchi nyingine. Kama ilivyo kwa kaya
na wafanyakazi, makampuni pia hukabiliwa na
gharama za juu za mijini. Uchambuzi wa nchi kwa nchi unathibitisha
kwamba viwanda vinavyozalisha katika majiji ya Afrika hulipa mishahara
ya juu zaidi kwa vigezo vya thamani halisi ya pesa kuliko makampuni
katika miji ya nchi nyingine ambazo ziko katika viwango
sawa vya maendeleo.
Ili
kujenga miji ambayo inafanya kazi—miji ambayo watu huweza kuishi,
inayofikika, yenye unafuu wa maisha, na hivyo kuwa na uchumi
imara—watunga sera watahitaji kuelekeza nguvu
zao katika matatizo ya ndani zaidi ya kimfumo, ambayo hayatengi ardhi,
yanavuruga maendeleo, na kukwaza tija.
“Ili
kuhakikisha ukuaji uchumi na maendeleo ya kijamii, miji inahitaji isiwe
ya gharama kubwa kwa makampuni na iweze kuwavutia zaidi wawekezaji,” anasema
Punam Chuhan-Pole, Kaimu Mchumi Mkuu, Benki ya Dunia katika Afrika na mtunzi wa ripoti hii.
“Pia ni lazima iwe inawajali wakazi, kuwapatia huduma, mahitaji. Yote
haya yatahitaji kufanya maboresho ya masoko ya ardhi ya mijini na kanuni
za miji na kuratibu
uwekezaji wa miundombinu katika hatua za awali.”
Vigezo vya biashara
Kushuka
kwa bei za bidhaa kumeshusha vigezo vya biashara vya Afrika kwa mwaka
2016 kwa takribani asilimia 16, wakati wasafirishaji wa bidhaa nje
wakipata hasara kubwa kwa bidhaa
zao. Katika bara zima kwa mwaka 2016, athari za mtikisiko huu
unatarajiwa kushusha ukuaji wa uchumi kwa asilimia 0.5 kutoka kwenye
msingi, na kudhoofisha mapato halisi na urari wa fedha kwa takribani
asilimia 4 na 2 juu ya msingi.
Kusonga Mbele
Nchi
za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara zitaendelea kukabiliwa na bei za
chini na zinazobadilika badilika katika masoko ya bidhaa duniani.
Serikali lazima zichukue hatua za
kujirekebisha kuja kwenye bei mpya za chini za bidhaa, kushughulikia
udhaifu wa kiuchumi, na kujenga vyanzo vipya vya ukuaji uchumi ulio
endelevu na jumuishi. Miji ya Afrika inayokua inatoa chachu ya kujenga
uchumi anuwai. Lakini inahitaji taasisi bora za
kupanga mipango athirifu na uratibu ambao utaweza kuinua wingi wa
shughuli za kiuchumi mijini na tija, na hivyo kuchochea mageuzi ya bara.
No comments:
Post a Comment